Hizi ndo sababu Za Ccm Kumtosa Wema

Chama cha Mapinduzi CCM kimeweka wazi sababu iliyowafanya wakatae kumpokea msanii Wema Sepetu kwenye chama hicho, ambaye hapo jana ametangaza kurudi kundini.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, kwanza amekanusha kumpokea mwanachama huyo na kusema kwamba, hakufuata utaratibu sahihi kuweza kurejea kwenye chama hicho ambacho alikiasi.
Pole Pole ameendelea kwa kusema kwamba CCM inajidhatiti katika kujijengea misingi imara na wanachama wake, hivyo wanataka mtu ambaye anaenda CCM awe amejidhatiti.
Pamoja na hayo Polepole amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kwamba msanii huyo ameshawishiwa kurudi CCM baada ya kuahidiwa atasaidiwa kumaliza kesi yake inayomkabili mahakamamni, pamoja na kunusuru kubomolewa kwa nyumba yao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment