Mkurugenzi TBA Akiri Picha Zinazosambaa Ni Zamajengo Ya Hosteli Hizo

Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi Elius A. Mwakalinga, amekiri picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya UDSM yana nyufa ni za majengo hayo, huku akisema ni kitu cha kawaida kwa majengo makubwa.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Mwakalinga amesema kutokea kwa nyufa hizo ni moja ya hatua za 'expansion joint' ambazo hutumiwa kwenye ujenzi wa majengo, lakini majengo hayo yamekidhi vigezo vyote na vipimo wakati wa ujenzi wake.

"Kila design tunayofanya ya majengo sasa hivi tunatumia expansion joint, majengo mengi makubwa huwa inatumia hiyo, hivyo ni common na sio creck kubwa sana kama inavoonekana kwenye picha, nilienda ile jana usiku kukagua tukakuta hiyo hali, ni process za majengo ili yaweze kusatle, hivyo watu wawe na amani kabisa wala wasiwe na hofu", amesema Bwana Mwakalinga.

Mwakalinga ameendelea kwa kusema kwamba watu wanaosambaza picha hizo bila kutaka ufafanuzi kutoka kwake wanafanya makosa kwani wanawatia watu hofu kwa jambo la kawaida kwenye hatua za ujenzi, huku wakilaumu kitu ambacho hawana uhakika nacho.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment