Kwa mujibu wa Microsoft asilimia kubwa ya benki katika nchi
zinazoendelea zinatumia programu ya Windows XP katika kuendesha ATM,
hivyo kuwa moja ya waathirika wa mpango huo.
Kwa ufupi
Dar es Salaam. Wiki moja kabla
ya kusitishwa huduma za programu ya kompyuta (OS) ya Windows Xp,
imefahamika kuwa waathirika wakubwa watakuwa ni benki na taasisi za
fedha ambazo hutumia mfumo huo katika mashine za kutolea fedha (ATMs)
Shirika la Microsoft limethibitisha kuwa benki ni miongoni mwa taasisi nyingi zitakazoathirika na mabadiliko hayo.
Baadhi zimeanza kufanyia kazi tatizo hilo, ikiwamo
benki moja ambayo jana alasiri ilituma ujumbe kwa wateja wake kuwa,
“Ndugu mteja, kuanzia Jumamosi saa 2:00 usiku Aprili 5, mpaka Jumapili
saa 12:00 asubuhi tutakuwa tunaboresha mashine zetu za ATM, hivyo kadi
yako haitafanya kazi kwa kipindi hiki. Asante.”
Kwa mujibu wa Microsoft asilimia kubwa ya benki
katika nchi zinazoendelea zinatumia programu ya Windows XP katika
kuendesha ATM, hivyo kuwa moja ya waathirika wa mpango huo.
Katikati ya Machi, Microsoft ilitangaza kusitisha
huduma zote zinazohusiana na bidhaa zake za Windows Xp kufikia Aprili 8,
mwaka huu. Pia shirika hilo litasitisha ufanisi wa programu ya kuzuia
na kupambana na virusi ya Microsft Security Essentials katika mfumo wa
Windows Xp, hivyo kufanya urahisi wa kompyuta zinazoitumia kukosa
ulinzi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Twiga Hosting, Jacob
Urassa alisema Watanzania hawatakiwi kupuuza onyo hilo kwa kuwa ikifika
Aprili 9 usalama wa taarifa zao utakuwa hatarini.
“Windows XP ni dhaifu mara tano zaidi ya Windows 7
na 8, kwa hiyo Microsoft wameona ni bora wakaitoa sokoni. Kwa maana
hiyo ATM na kompyuta zote zinazotumia programu hizo hazitakuwa na ulinzi
wa uhakika,” alisema Urassa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Teknolojia
ya Mawasiliano (IT).
Alisema kuwa kuna idadi kubwa sana ya Watanzania
wanaoendelea kutumia bidhaa hizo zikiwemo taasisi kubwa nchini hivyo
kuna haja kubwa ya kuchukua hatua za kubadilika na teknolojia.
Naye, Ofisa Uhusiano wa Benki ya Posta, Noves
Moses aliwatoa wasiwasi wateja wake kuwa licha ya kusitishwa kwa
matumizi ya Windows XP, bado benki hiyo itaendelea kutoa huduma zenye
kiwango kile kile.
- Kibadeni amfunika Logarusic
- Jinsi mabomu yalivyoua watu 6 Nairobi [VIDEO]
- Nchi itaingia kwenye historia ya dunia
- Askofu awaasa wajumbe kuheshimiana
- Dk. Gama alilia haki ya dini kwa watoto wa kike
- LHRC yataka Katiba ije na Sheria ya Ardhi
- Bavicha wapinga kauli za kuvunja Bunge
- ‘Ubunge wa Viti Maalumu ufutwe’
- Mtikila adai amezuiwa kuchangia bungeni
- Programu ya kompyuta kuvuruga ATM wiki ijayo
- Warioba amshukia Prof Shivji, asema ndiye chanzo cha uchochezi Zanzibar
- Sitta ampa barua Mtikila aende kwa JK
- Ukawa waanza mapambano nje ya Bunge
- Ajali mbaya yasababisha vifo vya watu 22 Rufiji
- Wajumbe wa Bunge Maalum wasusia Bunge
- Programu ya kompyuta kuvuruga ATM wiki ijayo
- ‘Shivji leo amebadilika sura kama kinyonga’ [VIDEO]
- Samata ang’ara, Al Ahly chali
- Kwa nini watu hupoteza hamu ya kujamiiana? -2
- Watu 12 wa familia moja wafa ajalini
- Nchi itaingia kwenye historia ya dunia
0 comments :
Post a Comment