Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana
na Profesa Sulochana Nair ,Makamu na Mtendaji Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Binary kilichoko Kuala Lumpur nchini Malaysia mara baada ya kuwasili
chuoni hapo tarehe 24.7.2015. Aliyesimama kushoto ni Profesa Joseph
Adaikalam, Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Chuo hicho.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA,
Mama Salma Kikwete akipokea TUZO maalum ya “ CWL International Women of
Excellency Award for Leadership” kutoka kwa Profesa Joseph Adaikalam,
Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Chuo Kukuu cha Binary kilichoko nchini
Malaysia kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika maendeleo ya
wanawake nchini Tanzania na Afrika tarehe 24.7.2015. Aliyesimama
(kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima,
akifuatiwa na Profesa Bulochana Nair na Kulia ni Profesa Datin Rohini
Devi wa Chuo Kikuu cha Binary.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akionyesha Tuzo Maalum aliyokabidhiwa na Profesa Joseph Adaikalam
(kulia) Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Chuo Kikuu cha Binary
kilichoko Kuala Lumpur nchini Malaysia na kushoto ni Makamu wa Mkuu wa
Chuo hicho Profesa Sulochana Nair tarehe 24.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akimkabidhi Tuzo Maalum aliyokabidhiwa na Uongozi wa Chuo Kikuu cha
Binary kwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima tarehe
24.7.2015.
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais,
Mama Salma Kikwete, akishuhudia utiaji saini (MoU) wa fursa za Binary
First Lady of Tanzania Scholarship kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu
Cha Binary. Wanaotia saini ni Ndugu Daud Nassib, Katibu wa WAMA na
Profesa Joseph Adaikalam, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Mtendaji wa Chuo
Kikuu cha Binary cha nchini Malaysia tarehe 24.7.2015. Kupita
makubaliano hayo Chuo Kukuu cha Binary kitatoa nafasi 10 za shahada za
uzamili.
Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Binary Profesa Joseph Adaikalam akibadilishana
hati za makubaliano (MoU) na Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,
WAMA, Ndugu Daud Nassib mara baada ya kutiliana saini makubaliano hayo
huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishuhudia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akitoa hotuba mara baada ya kutunukiwa Tuzo Maalum ya “ CWL
International Women of Excellency Award for Leadership’ na Chuo Kikuu
cha Binary kilichoko nchini Malaysia tarehe 24.7.2015.
Baadhi ya viongozi wa Chuo Kikuu
cha Binary na wqageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya tuzo na utiaji
saini ya Makubaliano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Binary
tarehe 24.7.2015 huko Kuala Lumpur nchini Malaysia.
PICHA NA JOHN LUKUWI.


0 comments :
Post a Comment