Sunday, July 26, 2015
@nkupamah blog
WATANGAZA nia watatu kati ya wanne wanaogombea Jimbo la Iramba mkoani hapa, wametangaza kugombea mchakato wa kura za maoni wakidai kuwa mgombea mwenzao Mwigulu Nchemba 'anabebwa' ashinde.
Wagombea hao; Juma Killimbah, David Jairo na Amon Gyunda walisema
mjini hapa jana kuwa, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa,
wanamfanyia kampeni za wazi Nchemba, ili apitishwe kuwa mgombea ubunge
kwa jimbo hilo.
Nchemba ni Naibu Waziri wa Fedha, aliyekuwa miongoni mwa wana CCM 38,
walioingia katika kinyang'anyiro cha kuomba chama hicho kiwachague
kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi wa Oktoba.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Killimbah alisema, wamekubaliana
kuchukua hatua hiyo endapo mchezo unaofanywa 'kumbeba' Nchemba
utaendelea na kuathiri demokrasia ya kugombea na kuchaguliwa kwa kura
halali.
Alisema kuwa, Msimamizi wa Uchaguzi katika kura hizo za maoni katika
jimbo hilo, Mathias Shidagisha na Msaidizi wake, Mwita Rahael walikuwa
miongoni mwa wanaombeba Waziri huyo.
Pia, alisema kuwa, mgombea mwenzao
huyo amekuwa akivunja kwa makusudi kanuni na taratibu za mchakato wa
kura za maoni, bila kuchukuliwa hatua yoyote.
Miongoni mwa mambo yanayo lalamikiwa ni pamoja na msimamizi huyo
kutumia gari la Nchemba kumsambazia mabango yake kwenda katika kata
mbalimbali.
Jambo lingine ni kitendo cha Msimamizi huyo kupita kwa makatibu kuwataka wahakikishe Nchemba anashinda.
Jambo lingine ni kitendo cha Msimamizi huyo kupita kwa makatibu kuwataka wahakikishe Nchemba anashinda.
@nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment