Sunday, July 26, 2015
@nkupamah blog
BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), limetishia kufungua kesi dhidi ya wamiliki wa magari watakaogoma na kusababisha usumbufu kwa wasafiri.
Tishio hilo limekuja baada ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania
(Taboa) kusema kuwa kitaitisha mgomo endapo serikali haitapunguza ushuru
wa mabasi kutoka asilimia 25 kufikia asilimia 10.
Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, Katibu Mtendaji wa Baraza
hilo, Dk Oscar Kikoyo alisema, wamepata taarifa ya mpango wa Taboa
kuitisha mgomo huo, nakwamba, kisheria chama hicho hakina haki ya
kufanya hivyo.
"Tumesikia kupitia vyombo vya habari kuwa utaitishwa mgomo. Tunaomba
ieleweke kuwa Taboa si chama cha wafanyakazi kwa hiyo, hakina haki ya
kuitisha mgomo wa wafanyakazi. Ni Chama cha Wamiliki wa Mabasi".
Aliongeza kuwa, endapo mgomo utaitishwa, utakuwa batili na wao
watakuwa na sababu ya msingi ya kumshitaki mmiliki mmoja mmoja alipe
fidia wasafiri kwa hasara watakayokuwa wameipata.
Katika hatua nyingine, alisema Sumatra inatakiwa kukunjua kucha zake
pia, kwa kuwachukulia hatua wamiliki hao wa mabasi, kutokana na
uchochezi wa migomo ya mara kwa mara. Ushuru unaolalamikiwa na wamiliki
wa mabasi ulianza kutozwa Julai Mosi, mwaka huu.
@nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment