Mhe. Emmanuel Nchimbi akitangaza mbele ya wanahabari kwa kutoridhishwa na maamuzi yao kamati kuu(CC). (Picha na Kajunason Blog)
Majina
yaliyopatikana, ambayo hata hivyo hayajatangazwa rasmi na chama, ni ya
Bernard Membe, Dk. John Magufuli, Dk. Asha Rose-Migiro, January Makamba
na Balozi Amina Salum Ali.
Membe
ni mbunge wa Mtama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Dk. Magufuli ni mbunge wa Chato na Waziri wa Ujenzi, Dk.
Migiro ni mbunge wa kuteuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Makamba ni
mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
na Balozi Amina ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Tume ya
Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Marekani.
Dk.
Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa wamefika mbele ya vyombo
vya habari mara tu kamati kuu ilipomaliza kikao chake usiku huu, na
kusema hawakubaliani na kilichotendwa.
Wajumbe
hao wakizungumza kwa kupokezana huku wakitoa kauli kali, wamesema
kanuni za utendaji katika vikao vilivyotangulia Kamati Kuu zimekiukwa.
Kamati Kuu ina wajumbe 32.
Wamesema
ukiukaji umekuja pale Kamati Kuu ilipopatiwa majina matano, badala ya
kupokea majina yote ya wanachama walioomba kuteuliwa, ili yenyewe ndiyo
itoke na majina matano baada ya kuyafanyia uchambuzi.
“Kanuni
zinasema Kamati Kuu itapokea majina ya waombaji wote na ikishafanya
uchambuzi wa kila muombaji, yakiwemo maoni ya kamati ya usalama na
maadili, ndiyo huchagua majina matano yanayofikishwa mbele ya
Halmashauri Kuu,” alisema Dk. Nchimbi ambaye alitokea kama kiongozi wa
hao wajumbe watatu.
Kimbisa
ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, amesema hawakubaliani na
maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu kwa sababu hawakutarajia Kamati Kuu
itakiukwa na kupokea majina ya baadhi tu ya waombaji.
“Haijawahi
kutokea tangu nilipoingia katika Kamati Kuu kushuhudia ukiukaji wa
kanuni kama ilivyotokea leo (jana) hii. Tumejitahidi kuuliza kwa
mwenyekiti imekuaje kanuni inakiukwa lakini tumekosa maelezo ya
kuridhisha,” amesema Simba, waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto.
0 comments :
Post a Comment