Friday, July 10, 2015
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa 12 wa watumishi wa
umma wa nchi za Afrika ambazo ni
wanachama Jumuiya ya Madola utakaonza Jumatatu ijayo jijini Dar es salaam.
Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimimwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete na kufungwa na
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dokta Ali Mohamed Shein
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma leo wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa Mkutano huo unatarajia utakaonza tarehe 13 na
kumalizika tarehe 15 unatarajiwa kujumuisha nchi 18 za Afrika ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya
Madola .
Bwana Mkwizu amezitaja
nchi hizo ni Botswana,Namibia,Cameroon, Ghana,Kenya,Lesotho,Malawi, Mauritius,Msumbiji,Namibia, Nigeria,Rwanda,Sychelles, Sierra
Leone,Afrika Kusini,Swaziland,Tanzania, Uganda,Uganda na Zambia.
Ameongeza kuwa wakati wa mkutano huo washiriki watapata fursa
ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoukabili utumishi wa umma wa nchi husika
na kubadilishana uzoefu ili kuimarisha utendaji na ufanisi katika utumishi wa
umma.
Aidha Kaimu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa wageni hao watapata
fursa ya kutembelea mji wa kihistoria wa
Bagamoyo,ili kuwapa fursa ya kujifunza
hazina kubwa ya kihistoria katika mji huo.
Hivyo , ametoa wito kwa wananchi wote kuonyesha moyo wa
ukarimu kwa wageni katika kipindi chote cha mkutano ili kuendeleza jina zuri la
Tanzania
0 comments :
Post a Comment