Sunday, July 26, 2015
@nkupamah blog
MBUNGE wa Jimbo la Tarime anayemaliza muda wake, Nyambari Nyangwine, amedai kuchezewa rafu akisema kuna baadhi ya vijana wamekuwa wakinywa pombe aina ya viroba kwa ajili ya kumzomea ili aonekane hakubaliki kutetea nafasi yake.
Nyangwine ambaye anatetea nafasi yake kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), sasa akigombea Tarime Vijijini, ametaka mchatako wa kumpata
mgombea ambaye atapeperusha bendera ya CCM kuwania ubunge katika jimbo
kufanyika kwa ustaarabu.
Alisema amelikemea jambo hilo katika vikao vya ndani huku akiwaomba
wagombea wenzake kuheshiminiana na kuongeza kuwa angependa uchaguzi uwe
huru na haki na kuwataka wagombea wenzake wasilazimishe kukubalika.
Hata hivyo, Nyangwine alisema ahadi alizitoa kwa wananchi wa Tarime
katika uchaguzi wa mwaka 2010 zimetekelezwa kwa asilimia zaidi ya 90 na
kwamba ana imani atashinda tena kwani wananchi wa Tarime wanaona kazi
kubwa ambayo ameifanya katika kipidi chake cha miaka mitano.
Nyangwine alisema endapo atateuliwa tena kuwania ubunge atahakikisha
CCM inapata ushindi wa kishindo katika Jimbo la Tarime Vijijini.
@nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment