Wafanyakazi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Marekani wakihakiki majina ya wageni waalikwa kwenye tafrija fupi ya
Ubalozi huo ya kumuaga Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulumula (hayupo pichani)
ambaye ndiye aliyekua Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Marekani. Tafrija hiyo fupi ilifanyika Alhamisi Julai 23, 2015 kwenye
jengo la Ubalozi lililopo mtaa wa 22, Washington, DC. Picha na Kwanza
Production na Vijimambo.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Balozi Donald Teitelbaum
mmoja ya wageni waliofika katika tafrija na aliyekua msemaji mkuu Balozi
Donald Teitelbaum ni Duputy Assistant Secretary for Afican Affairs.
Mshereheshaji Tuma akisherehesha kuagwa kwa Balozi Liberata Mulamula.
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama
Lily Munanka akisoma hotuba kwa niaba ya Maafisa na wafanyakazi wa
Ubalozi wakimtakia Balozi Liberata Mulamula Safari njema, kazi njema
kule aendako, daima tutakukumbuka na kazi nzuri ulioifanya kwa muda
mfupi uliokua nasi hapa Washington, DC daima itabaki kama kumbukumbu ya
ufanyaji kazi wako ambao ni mfano wa kuigwa. Hayo yalikua sehemu ya
maneno kwenye hotuba hiyo.
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama
Lily Munanka akimzawadia Balozi Liberata Mulamula zawadi kwa niaba ya
Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Balozi
Ramadhan Mwinyi akisoma hotuba ya kumuaga balozi Liberata Mulamula kwa
niaba ya Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York.
Balozi Donald Teitelbaum akisoma hotuba ya kumuaga Balozi Liberata
Mulamula kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani huku
akiwachekesha wageni waalikwa alipomalizia hotuba yake kwa kusema maneno
ya kiswahili " Balozi Liberata Mulamula ni kiboko" akiwa anamaanisha ni
mchapakazi.
Balozi Liberata Mulamula akitoa hotuba yake ya kuwaaga wageni
waalikwa wakiwemo Mabolozi, marafiki wa Tanzania na taasisi mbalimbali
zinazotangaza Tanzania nchini Marekani wakiwemo Maafisa na Wafanyakazi
wa Ubalozi na Jumuiya mbalimbali za Watanzania nchini Marekani
Wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Liberata Mulamula.
Picha ya pamona na Mabalozi na baadhi ya wageni waalikwa.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi


0 comments :
Post a Comment