@nkupamah blog
Afisa
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza na
madereva bodaboda wa Kipunguni ‘B’ kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa
Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote
anaweza kujiunga
Mkaguzi
Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat
Sylvery Tirumanywa akizungumza na wananchi mbalimbali waliofanikiwa
kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva
bodaboda wakiume maeneo ya Kipunguni ‘B’ katika manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam
Afisa
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma akitoa maelezo ya
kina kuhusu faida na huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa
katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na
kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi ya jamii ya (PSPF),
akiongea na madereva wa bodaboda wa Kipungunu ‘B’ wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva hao.
Delphin Richard Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akisalimiana na muamuzi wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Madereva wa Bodaboda wa Kipunguni ‘B’ ambapo mfuko wa PSPF imedhamini mashindano hayo. Katikati ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akitambulishwa wachezaji
Afisa
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliachi Remmy akisalimiana na
wachezaji katika ufunguzi wa ligi ya madereva bodaboda.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza mmoja wa wazee kuhusu Mfuko
wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote
anaweza kujiunga na kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi
ya jamii ya (PSPF)
Afisa
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma akimjazia fomu ya
Uchangiaji wa Hiari mmoja wa madereva wa Bodaboda wa Kipunguni B wilaya
ya Ilala jijini Dar mara baaada ya kupata elimu na kuridhia na huduma za
mfuko huo.
Madereva bodaboda wawana mwitikio mkubwa wa kujiunga na mfuko wa PSPF kupitia (PSS) kwakujaza fomu za Uchangiaji wa Hiari
Afisa
wa mfuko wa pensheni, Delphin Richard(kushoto) akimuonesha sehemu ya
kuweka alama ya dole gumba mmoja wa madereva wakati wa ujazaji fomu za
Uchangiaji wa Hiari
Afisa
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliachi Remmy(kulia)
akiwajazia fomu za Uchangiaji wa Hiari mmoja wa madereva wa Bodaboda wa
Kipunguni B wakati wa mashindano ya mpira wa miguu katika eneo la
Kipunguni B
……………………………………….
Madereva
bodaboda wa mtaa wa Kipunguni ‘B’ kata ya Kivule manispaa ya Ilala
wameanzisha ligi ya mpira wa miguu kwaajiri ya kuendeleza kujenga afya
zao kwa michezo kwani michezo ni afya kwa wote, wakati wa ufunguzi huo
wa ligi hiyo ya madereva bodaboda wadhamini wa ligi hiyo ambao ni Mfuko
wa pensheni wa (PSPF)nao hawakuwa mbali kwaajiri ya kuwawezesha madereva
hao kwa kipindi chote cha ligi hiyo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ligi hiyo mgeni rasmi ambaye ni mkaguzi
msaidizi wa polisi kanda maalumu ya dare s salaam Josephat Sylvery
Tirumanywa amewaasa madereva hao kuwa waweze kucheza kwa amani michezo
yote na pia waweze kuwa ni miongoni mwa watu watakao jiunga na na mfuko
wa (PSPF) ka kupitia (PSS) kwaajiri ya kuendelea kupata huduma zilizo
bora na zenye uhakika .
Pia Afisa masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Bw. Ismail Juma amesema wameamua kuungana na madeeva boda boda hao ili
kuweza kuwapa elimu katika suala la kuwekeza na kufaidika na mafao
mbalimbali yanayo tolewa na PSPF kwani Pindi watakapo jiunga na mfuko
huo wataona matunda mengi hasa kutokana na kuwa ni watu ambao
wanategemewa na familia zao hivyo kama Pspf wana mafao ambayo wataweza
kujikwamua kama mafao ambayo wanaweza kuwasomesha watoto,vilevile fao la
uzazi hata fau la nyumba pia ujiungapo na mfuko huu utafaidika na wala
hauto jutia
Naye Bw.Delphin Richard ambaye pia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa (PSPF) amewasisitiza
madereva kutii sheria za barabarani na pia kuweza kucheza ligi hiyo kwa
amani maana wamepewa dhamana ya kuwasafirisha abiria kwa amani na
upendo ,hivyo kati ya jeshi la polisi na madereva husaidiana kufanya
kazi kwa umoja na hivyo kuweka mahusiano mazuri katika kufanikisha nchi
yetu inajengwa na sisi watanzania kwa kuendeleza upendo na amani pindi
tuwapo barabarani,aliongeza kwa kuwapa shukrani madereva ya kuweza
kuchagua mfuko wa pensheni wa Pspf kuwa wadhamini wa michuano hiyo kwani
PSPF ipo kwaajiri ya kila mmoja na kuweza kuwaasa waweze
kuwahamasisha watu mbalimbali kuweza kujiunga na mfuko huo ili
kuhakikisha mabadiliko ya wananchi mbalimbali yanatokea kimaisha
,elimu,afya na mengine mengi.
Mfuko
wa pensheni wa PSPF unafuraha ya kuwa kwa sasa wananchi wanajua kile
kilicho sahihi nakuongeza kuwa wananchi mbalimbali waweze kufika maeneo
ya kipunguni B ilikuweza kushirikiana na madereva hao kwa kuwashangilia
wakati ligi ikiwa inaendelea na ligi hiyo itakayo dumu kwa takibani wiki
moja.
0 comments :
Post a Comment