
Katibu
Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza akiwahutubia
viongozi wa Wilaya, Majimbo na Matawi huko Ngoma Hazingwa Chakechake
Pemba.

Naibu
Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui akiwahutubia viongozi
wa Wilaya, Majimbo na Matawi kisiwani Pemba. (Picha na Salmin Said,
OMKR).
Na Khamis Haji , OMKR
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka
wananchi kisiwani Pemba watembee kifua mbele kwa sababu ni suala la
muda tu kabla hajatangazwa kuwa mshindi wa Urais wa Zanzibar na
kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya nane.
Maalim
Seif alisema hayo alipokuwa akihutubia katika mkutano ulioandaliwa kwa
ajili ya viongozi wa Wilaya, Majimbo na Matawi kisiwani Pemba
uliofanyika katika ofisi za uchaguzi za CUF Pemba zilizopo Ngoma
Hazingwa, Chakechake.
Alisema
wanachofanya viongozi wa CCM hivi sasa ni kuchelewesha muda tu, lakini
kwa kuwa wananchi wa Zanzibar wamemchagua yeye kuwa Rais na Dunia nzima
inafahamu hilo, hatimaye watamwita wenyewe na kumuapisha kuwa Rais wa
Zanzibar.
“Wananchi
wa Pemba kuleni mshibe, laleni bila ya hofu na tembeeni kifua mbele,
hawana njia lazima watakubali maamuzi ya wananchi wa Zanzibar
walionichagua niwe Rais wao”, alisema Maalim Seif.
Hata
hivyo, Maalim Seif alisema jambo la muhimu kwa wananchi wa Pemba na
Wazanzibari wote wasikubali kuchokozeka baada ya hali iliyojitokeza, kwa
sababu kuna watu lazima watafanya vitimbi kwa tama ya kuvuruga amani ya
nchi.
Alieleza
kuwa Chama cha Wananchi CUF kupitia Baraza Kuu la Uongozi tayari
kimeamua kwamba hakuna suala la uchaguzi wa Zanzibar kurejewa kwa sababu
wananchi wameshafanya maamuzi ya kidemokrasia katika uchaguzi uliokuwa
wa huru na haki.
Alisema
hakuna haja ya kupoteza muda na kuendeleza propaganda zisizokuwa na
msingi kinachopaswa kufanyika hivi sasa ni Tume ya Uchaguzi Zanzibar
kumalizia kazi yake na kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 25.
“Wache
wapoteze muda wataniapisha tu, na wajue muda wangu wa Urais utaanza
siku nitakapo apishwa kwa mujibu wa Katiba”, alisema.
Katibu
Mkuu huyo wa CUF ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
alisema jambo linalowatia kiwewe CCM na kutoa visingizio kuhusiana na
kura za Pemba ni kutokana na fedha nyingi walizotumia kwa tamaa ya
kupata majimbo kadhaa.
Alisema
kwamba CCM wamesahau kuwa miaka yote hawapati majimbo kisiwani Pemba na
hivyo si ajabu katika uchaguzi wa mwaka huu kukosa viti vyote vya
Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.
Maalim
Seif alisema hata huyo mgombea Urais wa Zanzibar kupitia ADC, Hamad
Rashid Mohammed ambaye alitegemewa na CCM kupunguza kura za Maalim Seif
kisiwani Pemba hakufua dafu na yeye mwenyewe (Hamad Rashid) aliambulia
kura 495 tu.
“Viongozi
wa CCM maskini walimdanganya sana Dk. Shein kuwa watapata viti Pemba na
kura za kutosha za Rais, wametumia fedha nyingi katika uchaguzi huu,
lakini walisahau hali halisi ya Pemba na sasa wanahangaika”, alisema
Katibu Mkuu wa CUF.
Alieleza
kuwa zipo taarifa kuwa kiasi cha shilingi milioni 70 zilitumiwa na CCM
katika jimbo moja tu la Mtambwe, jimbo ambalo katika chaguzi zote
zilizofanyika chama hicho hakijawahi kupata kura zaidi ya asilimia
tano.
Maalim
Seif aliwapongeza mawakala wa CUF katika majimbo yote 54 ya Zanzibar
kwa namna walivyo jidhatiti kulinda kura za chama chao na hatimaye
kukiwezesha kupata ushindi mkubwa ambao haujapata kutokea Zanzibar.
Naibu
Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazuri alisema uchaguzi mkuu
uliofanyika kisiwani Pemba mwaka huu ni mfano mzuri wa uchaguzi uliokuwa
huru na wa haki katika nchi nzima.
Alisema
kuwa wale wanaodai kuwa kura zimezidi kisiwani humo ni waongo wanaotapa
tapa kwasababu kuna watu waliojiandikishwa zaidi ya 200, 000 hawakupiga
kura na waliojitokeza kwenda kupiga kura ni 119,000.
Mazrui
alisema CCM wamepatwa na maumivu makubwa kisiwani Pemba kutokana na
matumizi makubwa ya fedha waliyoyafanya kwa tamaa ya kupata majimbo
manne, lakini wananchi wa Pemba hawakuona sababu ya kukichagua chama
hicho.
0 comments :
Post a Comment