Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea
nyaraka za Ofisi kutoka kwa Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo. Picha zote na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisaini
Kitabu cha wageni wakati alipoingia Ofisini kwake kwa mara ya kwanza baada ya
kukabidhiwa Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Nov
9, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal (kulia kwake), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula
na Naibu Katibu Mkuu wake, ....baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika
Ikulu jijini Dar es Salaam,leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa
Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, baada ya bakabidhiano
ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo

wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais Mama
Samia Suluhu Hassan na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa
Rais, wakati akiondoka baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu
jijini Dar es Salaam, leo.
Wafanyakazi
wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakiwa wamejipanga mstari wakisubiri kumpokea Bosi
wao Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwasili leo kwa mara
ya kwanza baada ya makabidhiano rasmi ya Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt.
Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea
zawadi ya Maua kama ishara ya makaribisho, kutoka kwa mfanyakazi wa Ofisi ya
Makamu wa Rais, Martha Mashuki, wakati alipowasili kwa mara ya kwanza kwenye
Ofisi yake na kupokelewa na wafanyakazi wake leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ua Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan,akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Sazi Salula,wakati
alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa ofisi
rasmi leo, Nov 9,2015. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Eng. Angelina Madete.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi yake wakati alipowasili kwenye
Ofisi yake kwa mara ya kwanza leo baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Makamu wa
Rais Mstaafu, Dkt. Bilal. Wafanyakazi hao walijipanga kumpokea huku wakiimba,
kupiga makofi na vigeregre wakati akiwasili.

akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati alipowasili
kwenye Ofisi hiyo leo Nov 9, 2015 baada ya makabidhiano. Akizungumza na
wafanyakazi hao Mama Samia, aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa
mashirikiano na kwa bidii ili kutimiza Kaulimbiu ya Mhe.Rais ya 'HAPA KAZI TU'.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Makamu wa Rais, Mama
Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza nao leo alipowasili Ofisini kwa mara ya
kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi rasmi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi
ya makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) alipowasili ofisi kwake kwa mara ya
kwanza leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi yake baada ya
kuzungumza nao alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wanamama wa Ofisi yake baada ya
kuzungumza nao alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza leo Nov 9, 2015 kwa
makabidhiano ya Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu.
0 comments :
Post a Comment