Thursday, December 3, 2015
@nkupamah blog
Waziri
mkuu, Kassim Majaliwa amefanya tena ziara ya kushtukiza bandarini na
shirika la reli Tanzania(TRL). Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji
na uingizaji mizigo bandarini.
Katika
maongezi ya awali meneja wa bandari alimuhakikishia kuwa mfumo
hauruhusu kontena kuibiwa lakini waziri mkuu alienda na ripoti ya
ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2431 bila
kulipiwa kodi.
Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu anawafahamu.
Katika
hatua nyingine, Waziri mkuu alitembelea shirika la reli na kukuta
mabilioni yametumika na miradi iliyokusudiwa haijatekelezwa.



0 comments :
Post a Comment