NYONI,Uswiz
Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA)
limewafungia Michel Platini na Sepp Blatter kujihusisha na shughuli
zozote za soka kwa kipindi cha miaka 8.
Sepp
Blatter ambaye alikuwa Rais wa Shirikisho hilo kabla ya kujiudhulu
wadhiwa huo mwezi wa sita
mwaka huu na Michel Platini akiwa Makamu wake.
Wamehukumiwa kutokana na kukutwa na hatia ya kukiuka maadili ya
shirikisho hilo kwa kuhusika na kupokea rushwa na matumizi mabaya ya
ofisi ,ambapo Kubwa zaidi ni malipo yaliyojaa utata (dola milioni 2 za
Kimarekani) aliyopokea Platini mwaka 2011 yaliyoidhinishwa na Blatter
Hata hivyo FIFA kupitia kamati yake ya maadili inayoongozwa na jaji Hans-Joachim Eckert
imewalima faini viongozi hao ambapo Blatter amelimwa faini ya dola
33,700 wakati Platin amepigwa faini ya dola 53,940 kama sehemu ya adhabu
hiyo
Hii
ina maana kuwa ndoto za Rais wa UEFA ambaye pia ni makamu wa Rais wa
FIFA.Michael Platin za kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi wa
shirikisho hilo uliopangwa kufanyika mwakani mwezi wa pili imeota mbawa
kutokana na kutakiwa kutojihusisha na soka katika kipindi chote cha
miaka 8 kuanzia leo.
Aidha
hali kama hiyo pia inamkuta Blatter ambaye alikuwa na tumaini la
kuachiwa huru katika kifungo cha awali cha siku 90 ili ashiriki katika
utoaji wa tuzo za mwanasoka bora wa dunia za Ballon D’or.
Hata
hivyo taarifa zinasema kuwa viongozi hao wamepewa nafasi ya kukata
rufaa kama wanaona hawajatendewa haki na kamti hiyo huru ya maadili.
0 comments :
Post a Comment