Rafiki wa karibu wa tabibu J.J,Mwaka, maarufu kama Lemutuz ambaye pia ni mtoto wa
aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Malecela ameeleza juu ya kinachoendelea kumuhusu rafiki yake huyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Lemutuz ameeleza kuwa anaimani kuwa anachokifanya Dkt Mwaka kimefuata sheria na taratibu za utabibu hivyo anasubiri taarifa kutoka wizarani ili kujua watatoa maamuzi gani.
Ameeleza kuwa Dkt Mwaka amekwisha ripoti wizarani akiwa ameambatana na vieelelezo vyote ambavyo serikali waliagiza aendenavyo, hivyo anaimani na kitakacho amuuliwa na wizara juu ya Dkt Mwaka.
Pia amewataka watu mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijaamii kutokushabikia vitu ambavyo havina ushahidi na kuwataka viongozi kujiridhisha kwanza kabla hawajaanza kutumbua majipu


0 comments :
Post a Comment