Tuesday, December 1, 2015
Mazungumzo ya kutafuta muafaka wa mgogoro wa kisiasa Zanzibar, yameendelea tena jana Ikulu Zanzibar.
Mazungumzo hayo yaliyowajumuisha viongozi watano wa kitaifa akiwamo Rais
wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim
Seif Sharif Hamad, yalichukuwa takriban saa sita. Mazungumzo hayo
yalianza saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni huku kukiwa hakuna
taarifa zozote zilizopatikana kilichofikiwa katika mazungumzo hayo.
0 comments :
Post a Comment