Sakata la Ufisadi wa Shilingi Trilioni 1.2 ......IKULU Yatoa Tamko,Yaitaka Stanbic Tanzania Ilipe Fidia ba Bilioni 13 Kwa Kufanya Udanganyifu

Tuesday, December 1, 2015

 @nkupamah blog

Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akiongea na Waandishi wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7 katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya Stanbink Tanzania.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7 katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya Stanbink Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bwana Assah Mwambene.

*********
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, leo amezungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam  kuhusiana na tuhuma zilizoelekezwa benki ya Stanbic Tanzania kuwa imetumika katika kufanya udanganyifu wa riba ya mkopo dola Milioni 600 (sawa  na Trioni 1.2 za kitanzania)  iliyopewa serikali ya Tanzania na Uingereza kupitia Kampuni ya Egma ya Tanzania.

Amesema kuwa Benki kuu ilipofanya ukaguzi wa benki hiyo na mambo mengine walibaini malipo yasiyokuwa ya kawaida kuhusiana na kampuni ya kitanzania inayoitwa Egma.
 
Sefue ameeleza kuwa malipo hayo yalikuwa kinyume na taratibu za kibenki na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walishindwa kuvumilia, hivyo tetesi hizo zikavuja.
 
Amesema baada ya tetesi kuvuja, wakaguzi wa benki kuu walifuatilia malalamiko hayo na kujiridhisha kuwa uongozi wa benki ya Stanbic Tanzania ulifanya mambo ambayo ni kinyume na taratibu zinazokubalika kibenki, ambapo fedha kiasi cha dola milioni 6 ziliingizwa kwenye kampuni ya Kampuni ya Egma na siku chache zilitolewa zote kwa fedha taslimu wala benki haikukusanya kodi ya zuio ambayo kwa mujibu wa sheria ya kodi ilipaswa kutozwa.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment