Mkuu wa huduma ya magereza katika mji Buenos Aires
Argentina amefutwa kazi baada ya
wafungwa watatu mashuhuri kutoroka
kutoka gereza lenye ulinzi mkali siku ya Jumapili.
Gavana wa jimbo hilo , Bi Maria Eugenia Vidal , alisema
yeye alichukua hatua hiyo kwa sababu kulikuwa na ushahidi kwamba
wafungwa wote walisaidiwa na maafisa wa idara ya magereza kutoroka .
Wafungwa hao Victor Schillaci na kaka wawili Cristian na
Martin Lanatta, walikuwa wanatumikia hukumu ya maisha gerezani kwa
makosa ya utekaji nyara na mauaji ya wafanyabiashara watatu katika tukio
lililohusishwa na mzozo wa madawa ya kulevya mnamo mwaka wa 2008.
Yamkini walitoroka kutoka kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi wakitumia bunduki bandia kutishia moja wa walinzi.
0 comments :
Post a Comment