Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Michael Mhando akifafanua jambo kwa
Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam(Hawapo Pichani).
Mkurugenzi wa Masoko, Elimu kwa
Umma na Utafiti Rehani Athumani akiongea na Waandishi wa Habari
(Hawapo pichani) kuhusu maboresho katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Waandishi wa Habari wakifatilia
taarifa iliyokuwa ikitolewa na Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) Leo Jijini Dar es salaam
Picha na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
……………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
unategemea kuboresha baadhi ya huduma zao ifikapo 2016 ili kuongeza
ufanisi katika utoaji wa huduma hizo kwa wananchi.
Akiyasema hayo leo Jijini Dar es salaam
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Michael Mhando amezitaja baadhi ya huduma ambazo
wana mpango wa kuziboresha kwa mwaka 2016 zikiwemo za kuongeza huduma
ya matibabu ya moyo kwa kutumia bima ya NHIF,kutoa mikopo ya
dawa,kurekebisha mfumo wa ulipaji wa baadhi ya huduma pia kubadili
gharama za huduma ambazo zinalipwa kwa watoa huduma ili kuendana na hali
halisi ya mfumuko wa bei.
‘’mimi binafsi nimefurahishwa na agizo la
Mheshimiwa Rais kutengeneza maduka ya dawa kila Hospitali ya Mkoa na
nitakua tayari kushirikiana nao kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya
kuhakikisha dawa zinapatikana wakati wote ili kuboresha huduma za afya
kwa wananchi’’alisema Mhando.
Naye Mkurugenzi wa Masoko, Elimu kwa Umma na
Utafiti Rehani Athumani amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili
zikiwemo za kukosekana kwa dawa katika hospitali husika pamoja na tabia
ya baadhi ya wanachama kugushi baadhi ya nyaraka wakati wa usajili.
Aidha,Bw. Rehani Athumani ametaja hatua
itakayochukuliwa ili kudhibiti ubora wa huduma zitolewazo na mfuko huo
kuwa ni kufanya ukaguzi wa kushtukiza ujulikanao kwa jina la kitaalamu
kama ‘Medical surveillance’ katika vituo vya matibabu ili kuona ubora wa
huduma wanazotoa kwa wananchi.
Katika kutoa huduma bora za afya kwa
wananchi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utahakikisha kuwa hatua kali za
kisheria zitachukuliwa kwa watoa huduma ambao wataongeza bei za huduma
kwa wanachama wa mfuko huo na maboresho hayo hayataathiri kiwango cha
michango kinachotolewa na wanachama.
0 comments :
Post a Comment