MUNICH.Ujerumani
Kocha wa Bayern Munich ya Ujerumani, Pep
Guardiola ataihama klabu hiyo atakapomaliza mkataba wake katika kipindi
cha majira ya joto. Bayern Munich imesema leo kuwa Carlo Ancelotti
atachukua nafasi yake
kama kocha mpya katika msimu ujao.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Karl-Heinz
Rummenigge ameliambia gazeti la kijerumani linalotoka Jumapili, Bild,
kwamba wanashukuru kwa yote yaliyofanywa na Guardiola katika klabu hiyo
na wana matumaini watapata mafanikio ya pamoja katika msimu huu.
Amesema
Ancelotti, kocha mwenye mafaniko anajiunga na Bayern Munich na
wamejiandaa kufanya naye kazi. Guardiola raia wa Uhispania anayetokea
jimbo la Catalonia, alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Jupp Heynckes mwaka
2013.
Aliifanikisha Bayern Munich kushinda
katika michuano ya Ligi Kuu ya Ujerumani-Bundesliga, Kombe la Shirikisho
la Ujerumani, Kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya na Kombe la Dunia la
FIFA.
0 comments :
Post a Comment