ARUSHA
Waziri wa mambo Nje Afrika Mashariki
kikanda na kimataifa balozi Dk Agustino Maiga amewaagiza wakurugenzi wa
mashirikia yaliyo chini ya wizara hiyo kuacha tabia ya kubuni miradi ya
muda mfupi isiyo na
tija kwa ajili ya kuwafurahisha viongozi au
waonekane kuwa wanafanyakazi na badala yake wajenge miradi ya kudumu
yenye maslahi kwa taifa na kizazi kijacho hata kama utekelezaji wake
utachukua muda mrefu.
Balozi Agustino Maiga ametoa kauli
hiyo jijini Arusha katika ziara ya kukagua miradi inayo tekelezwa na
wizara ya mambo ya nje ambaye ilianzia katika kituo cha mikutano cha
kimataifa cha AICC na ujenzi wa kituo cha kumbukumbu ya iliyokuwa
mahakama ya kimbari ya Rwanda kinachojegwa jijini Arusha na kutoa agizo
ilo kwa wakurugenzi wa mashihirika yaliyo chini ya wizara hiyo.
Mkurungenzi mtendaji wa kituo cha
kimataifa cha AICC Elishiria Kaaya amesema AICC imewapokea maagizo ya
waziri na tayari ilishaanza kutekeleza miradi imara na sasa kwa
kushirikiana na wizara ya nishati na madini wanajenga kituo kikubwa cha
madini kitakacho hifadhi na kuchakata madini ya vito bila kupeleka nchi
za nje.
0 comments :
Post a Comment