Katika
kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya
Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa
Septemba 2015.
Mshindi
wa mwezi wa Oktoba, 2015 ni Mohamed Hussein Tshabalala ambapo amepata
kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka
wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na
huduma ya Simba News.
Akikabidhiwa
tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mwanachama na Shabiki wa
Simba Mbunge wa Busega Simiyu Mh. Raphael Chegeni, beki wa kushoto
Mohamed Tshabalala alisema “tangu nilipotata taarifa za kushinda tunzo
ya mchezaji bora kwa mwezi wa 10 nilifurahi sana na leo furaha yangu
inazidi zaidi, kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuwa
mchezaji na kuweza kushinda tunzo hii, pili kuushukuru Uongozi na
wapenzi wa Simba walioona mchango wangu kwenye kikosi cha Simba na
kunipigia kura kwa wingi na mwisho napenda kushukuru familia yangu
pamoja na watu wangu wote wa karibu ambao wamekuwa mchango mkubwa kwenye
mafanikio yangu ya soka”. Ninachoweza kuwaahidi ni kuwa kamwe
sitowaangusha kwani tunzo hii itakuwa chahu katika mafanikio yangu
aliongeza Tshabalala.
Mwanachama
na Shabiki wa Simba Mh. Chegeni alisema “kwanza kabisa nashukuru kwa
Simba kunipa heshima ya kuweza kuwa mgeni rasmi katika kutoa tunzo hii
kwa Tshabalala, napenda kumshauri Tshabalala na wachezaji wetu wengine
kuendelea kujituma kwa bidii kwa ukiweka nidhamu, kujituma na kufanya
kazi kwa bidii ni lazima mafanikio utayapata”.
Akizungumza
leo jijini Dar es salaam Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Uongozi,
wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji
katika kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la
busara kuwa klabu ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tunzo za mchezaji
wake bora. Tunaamini kuwa Tunzo ya Mchezaji bora wa mwezi wa Simba
itaongeza ari na kujituma kwa wachezaji wetu. Sisi tukiwa kama viongozi
ni kazi yetu ya msingi kuhakikisha kuwa wachezaji wetu hasa wale
wanaojituma zaidi wanatambuliwa na kuenziwa’’.
Akizungumza
jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG
Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba,
Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo
ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la
mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao
wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na Tigo wataweza kupiga
kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba’’
Tukumbuke
kuwa unaweza kumchagua mchezaji bora wa mwezi ukiwa umejiunganisha na
huduma ya Simba News kwa kutuma jina la mchezaji kwenda namba 15460.
Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa October, 2015 linaanza
tarehe October 10, 2015. Piga kura mara nyingi zaidi kuweza kumpata
mchezaji wako bora wa Mwezi October, 2015.
Simba
News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba
habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya
wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya
Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni
maalum kwa Tigo na Vodacom.
0 comments :
Post a Comment