Wafuasi wa CCM na UKAWA Wachapana Makonde Wilayani Masasi

Wednesday, December 2, 2015

  @nkupamah blog

Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wilayani Masasi, mkoa wa Mtwara wamechapana makonde kufuatia mzozo wa kisiasa ulioibuka kati ya vyama hivyo.

Kufuatia vururugu hizo, polisi waliingilia kati na kufyatua risasi hewani kuwatawanya.

Wafuasi hao walichapana makonde pamoja na kurushiana mawe jana katika maeneo ya T.K, kwenye barabara kuu iendayo mjini Newala wakati walipokuwa wakitoka katika mikutano ya kampeni ya wagombea wao wa ubunge inayoendelea kwa ajili ya uchaguzi mdogo kwenye jimbo hilo.

Mashuhuda wa vurugu hizo wamesema  kuwa  vurugu hizo zilitokea baada ya kundi la wafuasi wa UKAWA waliokuwa wakitoka katika mkutano wa mgombea ubunge wa Cuf, Ismael Makombe, kwenye viwanja vya Mti Mwiba alikokuwa akifanya mkutano wake na kurejea majumbani, kukutana uso kwa uso na wafuasi wa CCM   maeneo ya T.K  ambapo walianza kuzozana juu ya sifa walizonazo wagombea wao.

Taarifa zaidi zinaarifu kuwa baada ya mzozo huo wafuasi hao walianza kupigana na kurushiana mawe mazito ikiwamo matofali na kupelekea baadhi kupata majeraha kwenye maeneo mbalimbali ya miili yao na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Inaarifiwa kuwa T.K ni kijiwe ambacho kinatumiwa na wafuasi wa CCM kukaa na kufanya shughuli zao mbalimbali za kujiingizia kipato, lakini tangu kampeni zianze hasa mikutano inapokuwa imeisha saa12:00 jioni, wafuasi wa Ukawa wamekuwa wakipita eneo hilo huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kukibeza CCM pamoja na mgombea wake Rashidi Chuachua.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment