Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama
wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (kushoto) akimshukuru
kwa kukaribishwa vizuri nchini pamoja na ushirikiano waliofanya baada ya
kusaini kusaini Hati ya Makubaliano mwanzoni mwa wiki hii katika hafla
iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya
Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (kushoto) wakati
alipomsindikiza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya kumuaga kiongozi huyo wa China. Naibu Waziri
huyo wa China na Waziri Kitwanga, mwanzoni mwa wiki hii walisaini Hati
ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kulia) akifurahi jambo na Naibu Waziri wa Wizara ya
Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang (kushoto) wakati
walipokuwa wanaagana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam leo.. Naibu Waziri huyo wa China na Waziri
Kitwanga, mwanzoni mwa wiki hii walisaini Hati ya Makubaliano ya
ushirikiano kati ya wizara hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kulia) akimuaga kwa kumpungia mkono Naibu Waziri wa
Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang
(kushoto ndani ya gari) wakati kiongozi huyo wa China akiwa anaondoka
mara baada ya kumaliza ziara yake nchini. Juzi Waziri Kitwanga na Naibu
waziri huyo wa China walisaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika
masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama wa Raia kati ya Wizara hizo
mbili, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara
hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri Kitwanga ni Mkuu wa Utawala
wa Jeshi la Polisi, Kamishna Thobias Andengenye

0 comments :
Post a Comment