Mgogoro wa Zanzibar
……..
Mosi, Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu atangazwe haraka ili hali ya utulivu wa kawaida irejee. Mshindi ale kiapo, aunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuwaunganisha Wazanzibari.
Mosi, Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu atangazwe haraka ili hali ya utulivu wa kawaida irejee. Mshindi ale kiapo, aunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuwaunganisha Wazanzibari.
Pili, ACT-Wazalendo imebaini kuwapo kwa
idadi kubwa isivyo kawaida ya wanajeshi wanaolinda Bandari, Uwanja wa
Ndege, Vituo vya Redio na
maeneo mengine muhimu. Chama chetu kinataka
askari hao warejee makambini kwao kwani uwepo wao katika maeneo ya
kiraia unasababisha hali ya shaka na hofu miongoni mwa wananchi.
Tatu, kwa ajili ya mustakabali mwema wa
Zanzibar, ACT-Wazalendo kinataka mazungumzo yoyote kuhusu uchaguzi
uliofutwa yahusishe wadau wa vyama vyote na taasisi nyingine
walioshiriki kwenye uchaguzi.
Hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa
vyama vya CCM na CUF kukutana na kufanya mazungumzo baada ya kutokea
matatizo. Lakini uzoefu unaonyesha kwamba suluhisho huwa si la kudumu na
badala yake matatizo yaleyale hujirudia baada ya muda.
Suluhisho la hali hii ni vyama vingine
vyote, kujumuishwa katika aina hii ya mazungumzo ili kupata mawazo
jumuishi na yatakayowakilisha sehemu kubwa zaidi ya Wazanzibari ambao
wengi wao, hasa kizazi kipya, hawana uhusiano wowote na vyama hivyo
viwili.
Kwa ujumla hali ya kisiasa Zanzibar ni
mbaya sana na inatisha kwani wananchi wanaishi kwa hofu kubwa na
hawaelewi kinachoendelea, ukimya uliotamalaki hauashirii hatima njema ya
siasa za Zanzibar.
ACT-Wazalendo kinapenda kutumia nafasi
hii kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa subira na
uvumilivu wa kiwango cha juu waliouonyesha katika kipindi hiki cha hali
ya sintofahamu.
Imetolewa leo, Desemba 20, 2015.
Mji Mkongwe, Zanzibar
Kabwe Z Ruyagwa Zitto, Mb
Kiongozi wa Chama
0 comments :
Post a Comment