ZITTO KABWE AAPA KUFA NA SAKATA LA ESCROW KWA MTINDO HUU

@nkupamah blog

DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Mjini,Zitto Kabwe amesema kuwa atahakikisha wakati wa vikao vya  bunge vitakavyoanza mwakani anaibana Serikali juu ya baadhi ya mambo hasa katika ufafanuzi juu ya
lililokuwa sakata la Tegeta Escrow.
Zitto kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook amefichua kuwa atahakikisha anapambana ili suala hilo linajibiwa kikamilifu na kwamba pesa zote ambazo Serikali inawadai wamiliki wa mitambo ya IPTL zinarudishwa kwa wananchi
“Juzi nimewasilisha maswali 5 Bungeni ili yajibiwe na Serikali. Swali la kwanza linahusu umiliki wa IPTL na tshs 8 bilioni tunazowalipa matapeli hao kila mwezi, kwanini mtambo haujamilikishwa TANESCO na anayejiita mmiliki wa IPTL kukamatwa na kushtakiwa. Vile vile ni kwanini Benki ya Stanbic haijachukuliwa hatua kwa kuamuriwa kurudisha Fedha za akaunti ya ‪#‎TegetaEscrow‬. Mambo 2 ( umiliki wa IPTL na kurudisha kwa fedha tshs 320 bilioni) ndio mambo ya msingi kabisa katika suala zima la #TegetaEscrow. Haya ndio nitakufa nayo.”
Juzi nimewasilisha maswali 5 Bungeni ili yajibiwe na Serikali. Swali la kwanza linahusu umiliki wa IPTL na tshs 8
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment