Na Ramadhan Ali Maelezo-Zanzibar
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanz
ibar (ZSTC) Bi. Mwanahija Almasi Ali amesema Shirika hilo lina fedha za kutosha kununua karafuu zote kutoka kwa wakulima kwa fedha taslimu na hakuna mpango wa kununua karafu zao
kwa njia ya mkopo.ibar (ZSTC) Bi. Mwanahija Almasi Ali amesema Shirika hilo lina fedha za kutosha kununua karafuu zote kutoka kwa wakulima kwa fedha taslimu na hakuna mpango wa kununua karafu zao
Akizungumza na Waandishi wa
Habari Ofisini kwake Maisara, Bi. Mwanahija alikiri kuwa msimu huu wa
vuli zao la karafuu limekuwa kubwa kinyume na walivyotaraji lakini
wamejipanga na wanazo fedha za kutosha.
Taarifa ya Mkurugenzi Mwendeshaji
wa ZSTC imekuja kufuatia baadhi ya wadau wanaojishughulisha na zao la
karafuu kuvumisha kuwa wanapofika vituoni kuuza karafuu hupewa risiti
na kutakiwa wakae siku tatu hadi wiki moja ili wakachukue fedha zao.
“Wananchi wanaojishughulisha na
zao la karafuu wanatoa taarifa zisizo sahihi kwa ZSTC kuwa hatuna fedha
na wanapokwenda kuuza karafuu vituoni hupewa risiti na kutakiwa
wasubiri wiki moja wapatiwe pesa, taarifa hiyo sio sahihi, ” alisema Bi
Mwanahija.
Alisema ZSTC ni Shirika
linalofanya biashara na linaruhusiwa kwa mujibu wa sheria kukopa
Taasisi za kibenki kwa ajili ya kukidhi gharama za kununulia karafuu
kutoka kwa wakulima iwapo msimu wa zao hilo umekuwa mkubwa.
Ameongeza kuwa iwapo kima cha
fedha watakazokopa kimekuwa kikubwa kupita kiwango kinachokubaliwa na
Taasisi za fedha kukopa wanaweza kutoa taarifa Serikalini na ikawapa
fedha kuendelea kununua karafuu za wakulima.
“Mpaka sasa hivi hatujakuwa na
shida ya kukopa kutoka Taasisi za kifedha wala kutoa taarifa Serikalini
kupata fedha za ziada kwa sababu tunazo za kutosha na tumejipanga,
”alisisitiza Mkurugenzi Mwendeshaji ZSTC.
Alisema wakati msimu wa uchumaji
karafuu za vuli upo katikati, katika wiki ya kwanza ya mwezi Disemba
Shirika limenunua tani 236 za karafuu zenye thamani ya shilingi bilioni
3.3 , wiki ya pili tani 379.7 zenye thamani ya shilingi bilioni 5.315
na wiki ya tatu wamenunua karafuu zenye thamani ya shilingi bilioni
7.2.
Kuhusu kuliendeleza zao la
karafuu Zanzibar, Bi. Mwanahija Almasi alisema Serikali kwa kutambua
umuhimu wa zao hilo imeanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu ambao lengo
lake kubwa ni kutoa visaidia kwa wakulima.
Alivitaja visaidizi hivyo kuwa ni
pamoja na kuwapatia wakulima miche bila malipo, kuhamasisha wananchi
kuanzisha vitalu vya miche ya mikarafuu na kuwapa mikopo wakulima
wakati wa maandalizi ya kuchuma zao hilo .
“Msimu huu wa vuli Shirika
limetoa mikopo kwa wakulima wa karafuu 126 Unguja na Pemba yenye thamani
ya shilingi milioni 34,” Mkurugenzi aliwaeleza waandishi wa Habari.
Akizungumzia mwamko wa wakulima
wa karafuu kuweka fedha Benki baada ya kuuza karafuu zao ili kujiepusha
kuibiwa alisema pamoja na juhudi wanazochukua kuwapa taaluma juu ya
suala hilo bado muitikio haujawa nzuri kwa wakulima wengi.
Amesema wakulima wengi wa karafuu
wanapenda kukaa na pesa zao majumbani ili kupata urahisi wa kuzitumia
wanapozihitaji pamoja na tishio la tatizo la wizi ambalo katika msimu
wa karafuu limekuwa kubwa.
0 comments :
Post a Comment