Nkupamah media:
Azam FC.
Ikitoka nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, timu hiyo ya Chamazi
ililamizika kufanya kazi ya ziada kwenye uwanja wenye changamoto ya
mashimo wa Ushirika.
Kikosi cha Wanalambalamba kilichoanza na nyota wanne wa kigeni;
beki wa kati Serge Wawa, kiungo Michael Bolou na washambuliaji Didier
Kavumbagu na Allan Wanga kilazimika kusubiri hadi dakika ya 63
kusawazisha bao la dakika ya 48 lilofungwa na beki Godfrey Mbuda.
Beki wa kimataifa kutoka Ivory Coast, Wawa ndiye aliyefufua
matumaini ya Azam FC akifuta makosa ya safu ya ulinzi kwa kumalizia kwa
kichwa cha kuparaza mpira wa kona iliyopigwa na beki pembeni kulia,
Erasto Nyoni kutoka kusini mashariki mwa Uwanja wa Ushirika.
Nyoni alipiga kona nyingine murua katika dakika ya 77 ambayo
iliwababatiza mabeki wa Panone FC kabla ya kukwamishwa nyavuni kwa shuti
'mtoto' la mguu wa kulia na straika Mkenya, Wanga.
Kwa ushindi huo, Azam imeunga na timu sita za Ligi Kuu - Coastal
Union, Ndanda, Prisons, Mwadui, Simba na Yanga pamoja na timu pekee ya
Ligi Daraja la Kwanza, Geita Gold kukamilisha orodha ya timu nane
zitakazochuana kwenye hatua ya robo-fainali
Bingwa bingwa wa michuano hiyo ambaye ataiwakilisha Tanzania Bara katika Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.


0 comments :
Post a Comment