Nkupamah media:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Masamaki na wenzake wanakabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi,
ikiwamo kuidanganya serikali na kuisababishia hasara ya Sh. bilioni
12.7.
Hatua hiyo imefikiwa jana na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi,
baada ya ZCO kuwasilisha maombi ya kuendelea kuwahoji washtakiwa hao,
ofisini kwake.
Hakimu Shahidi alisema amepokea barua ya kuomba kibali cha kwenda
kuwahoji tena washtakiwa lakini haijaeleza kuhusu nini na kwamba
mahakama yake haina pingamizi.
Mbali na Masamaki, washtakiwa wengine ni Meneja wa Kitengo cha
Huduma za Ushuru, Habibu Mponezya (45), Burton Kaissy (51), Msimamizi
Mkuu wa Bandari Kavu ya Azam (ICD – Azam), Eliachi Mrema (31), Mchambuzi
Mwandamizi wa Biashara TRA, Khamis Omary (48), maofisa wa Kitengo cha
Mawasiliano ya Kompyuta (ICT – TRA), Haroun Mpande (28), Raymond Louis
(39) na Ashraf Khan (59) wote wakazi wa jijini.
Jana, Wakili wa Serikali Esteria Wilson, alidai mahakamani kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa
Serikali Mkuu Timon Vitalis, uliwasomea washtakiwa hao mashitaka yao.
Alidai kuwa kati ya Juni Mosi na Novemba 17, mwaka jana, siku
isiyofahamika, washitakiwa walikula njama ya kutenda kosa la kuidanganya
serikali.
Ilidaiwa kuwa walikula njama kwamba makontena 324 yailiyokuwa
bandari kavu ya Azam yametolewa baada ya kulipiwa kodi huku wakijua si
kweli.
Vitalis alidai katika shitaka la pili siku na tarehe ya tukio la
kwanza, washtakiwa wote kwa pamoja walishindwa kutimiza majukumu yao na
kusababishia serikali hasara ya Sh. Bilioni 12.7.
Hakimu Shahidi alisema kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya
kusikiliza kesi za uhujumu uchumi, washtakiwa hawakutakiwa kujibu
chochote hadi upelelezi utakapokamilika na kuhamishiwa Mahakama Kuu
Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Washtakiwa waliwasilisha maombi ya dhamana Mahakama Kuu na wako nje kwa dhamana.
Novemba 27, mwaka jana, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara
ya kwanza ya kikazi na ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam na
kuibua kashfa hiyo ya wizi wa makontena na ukwepaji wa kodi wa Sh.
bilioni 80.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alikutana na viongozi waandamizi wa
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na TRA na kubaini wizi wa
makontena 349 uliotokana na ukwepaji wa kulipa kodi.
0 comments :
Post a Comment