BEN POL NA JUX WAPEANA MAKAVU KWENYE ‘NAKUCHANA’

nkupamah media:

unnamed (1)
Ujumbe wenye dalili za ukweli uliojificha ndani ya mzaha umezaa wimbo mkubwa kati ya wakali wawili wa RnB Tanzania, Benard “Ben Pol” Paul
na Juma “Jux” Khaleed.
‘NAKUCHANA’ ni wimbo mpya wa RnB ambao ndani yake Ben Pol na Jux wanasikika wakipeana ‘makavu’ kuhusu mambo kadhaa hasi kuhusu wao, huku kila mmoja akitafuta kile anachoamini ni kona dhaifu ya mwenzake.
“Nakuchana ilizaliwa baada ya mimi na Jux kwenda studio, na tulienda studio tulitaka kwenda kurekodi kabisa wimbo rasmi, lakini tukawa tunajivuta vuta, tukaona bana eh hebu lets just have fun umeona, sababu tulikaa muda mrefu kama masaa matatu hatujapata kitu. Kwahiyo tukasema ngoja tujifurahishe (kwa kuchanana) kama watu ambao wanakuwa wana have fun wanavyochill sehemu, unajua wanazinguana  wanafanyaje. Kwahiyo kwenye ku-
have fun ndio tukaandika mstari mmoja mmoja tunau record, tunaandika mmoja tunau record yaani tumeandika  yote kwa pamoja. Kwahiyo hivyo ndivyo ambavyo ‘Nakuchana’ ilivyozaliwa.” Alieleza Ben Pol kuhusu wimbo huo.
Ben Pol ameongeza kuwa wamelazimika
kuitoa ‘NAKUCHANA’ kipindi hiki kutokana na  demo ya wimbo huo kuvuja siku chache baada ya kurekodiwa na kuonekana kupendwa na mashabiki wengi.
‘NAKUCHANA’ ni wimbo uliopikwa
na producer Bob Manecky wa studio ya A.M Records, na ndio collabo ya kwanza kwa Jux na Ben Pol kufanya.
PS: Wimbo wa ‘NAKUCHANA’ umeambatanishwa kwenye barua pepe hii, tafadhali usambaze na kwa wengine.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment