Nkupamah media:
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
Matokeo hayo ya kupangwa, yalizihusisha Geita Goldmine FC ya Geita
iliyoibamiza JKT Kanembwa ya Kigoma mabao 8-0, wakati Polisi Tabora
wakiifunga JKT Oljoro ya Arusha mabao 7-0. Mechi hizo zilichezwa
Februari 13 mwaka huu.
Bosi Malinzi alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye
Ofisi za TFF kuhusu hatma ya upangaji huo matokeo ambao sasa
utajadiliwa na kamati ya nidhamu.
Kabla ya kutoa lugha hiyo kali (tunahifadhi) na isiyozoeleka kwake,
Malinzi aliulizwa swali: “Katika suala hili la Geita, unatajwa kuhusika
na upangaji matokeo na ulikuwa ukifanya mawasiliano na viongozi wa timu
mojawapo?.”
Akijibu tuhuma hizo, bosi Malinzi aliwaka na kutoa matamshi makali, ambayo yalisababisha pia mkutano kuvunjika.
"Naendesha taasisi kubwa kama hii, ninawezaje kuhusika na suala la kupanga matokeo?,” alifoka Malinzi na kuongeza:
“Kama nahusika na kuna mtu ana ushahidi, aende polisi hata leo hii
kufungua mashtaka. Kuna mchezo unachezwa hapa, ninajua kila
kinachoendelea na wote nawafahamu.”
Alisema tangu kumalizika mechi hizo mbili, yeye binafsi na TFF wamekumbana na matamshi ya shutuma.
“Nimekaa kimya kwa sababu suala hili liko mikononi mwa vyombo husika kufanya uchunguzi na kutoa uamuzi.
"Nimetukanwa sana kwenye mtandao wa Jamii forum, redioni, facebook.
Nafahamu zilikoanzia shutuma hizi, lakini niwahakikishie watu hao kuwa
hawatafika kokote.”
Hata hivyo, Malinzi alisema TFF imebaini kuwapo viashiria vya
upangaji matokeo kwenye mechi hizo na wahusika wanatarajiwa kufikishwa
mbele ya vyombo vya sheria Machi 20 mwaka huu.
Alisema Sekretarieti ya TFF inaandaa mashtaka kuhusiana na kesi hiyo na wahusika wote watajulishwa.
“Jambo hili ni kubwa sana na baada ya kuona kanuni kwenye Kamati ya
Mashindano hazijitoshelezi, tumeamua kulipeleka Kamati ya Nidhamu.
"Siku zote Fifa, Caf, TFF zinapiga vita upangaji wa matokeo, katika hili TFF ni walalamikaji na tutaeleza ya kwetu.


0 comments :
Post a Comment