Nkupamah media:
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro,
alisema jana kuwa mwanamke huyo (jina linahifadhiwa kwa sababu za
kiuchunguzi), anashikiliwa na watuhumiwa wengine wanne ambao walikuwa
wakishirikiana kufanikisha wizi huo.
Sirro aliwataja watuhumiwa wenzake kuwa ni Mohamed Hassan (21)
maarufu kama Kidali, mkazi wa Vingunguti Spenko, Adam Salum (23) mkazi
wa Buguruni kwa Madenge, Hamis Ally (20) na Bakari Hamis (19) wote
wakazi wa Buguruni kwa Mnyamani.
Alisema watuhumiwa hao ambao wamekuwa wakifanya unyang’anyi wa
kutumia silaha, walikamatwa Alhamis iliyopita eneo la Buguruni kwa
Mnyamani.
Kamishna Sirro alisema mwanamke huyo amekuwa akienda benki na kukaa
humo kama mteja kisha kuangalia mteja anayetoa kiasi kikubwa cha fedha
na kuwasiliana na watuhumiwa wenzake ili kufanikisha uporaji.
“Amefanikisha matukio mengi ya unyang’anyi wa kutumia silaha katika
benki tofauti. kazi yake ni kukaa ndani ya benki kama mteja na
kuangalia wale wanaotoa fedha nyingi kisha kuwasiliana na wenzake wa
nje,” alisema.
Aliongeza kuwa: "Yapo matukio mengi ambayo ameyataja kuwa aliyafanikisha kutendeka. Tunaendelea na uchunguzi.”
Alisema watu hao walikamatwa baada ya polisi kupata taraifa kutoka
kwa msiri wao kuwa kuna majambazi yanajiandaa kuvamia maduka eneo hilo.
"Watuhumiwa walikiri kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu wa
kutumia silaha. Mojawpao ni tukio lililotokea Februari 14, mwaka huu,
huko Ivan Min Supermarket. Juhudi za kuitafuta silaha waliyoitumia
zinaendelea", alisema.
Kamishna Sirro alisema mwishoni mwa wiki iliyopita, wamefanikiwa
kuzikamata silaha mbili aina ya SMG iliyokatwa mtutu yenye namba
56-1-2803795 ikiwa na risasi 24 kwenye magazini.
Nyingine aliitaja kuwa ni bastola aina ya Browning yenye namba A
671123 na TZ CAR 98580 ikiwa haina risasi kwenye na magazini ambayo
haina risasi.
Alisema silaha aina ya SMG ilipatikana baada ya kukamatwa watu
wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi, waliokuwa wakikimbia baada ya
kufanya uporaji wa Sh. milioni 12.
Alisema fedha hizo ambazo ni mali ya David Isack (32), mkazi wa
Mafinga mkoani Iringa, ambaye wakati wa tukio, alikuwa akitoka benki ya
NMB tawi la Airport kuzipeleka benki ya DTB, jengo la Quality Plaza,
barabara ya Nyerere, Dar es Salaam.
Alisema wakati yuko njiani, alivamiwa na watu watano waliokuwa
kwenye pikipiki mbili aina ya Boxer na kumpora begi lenye fedha kisha
kupiga risasi mbili hewani.
Alisema baada ya polisi kupata taarifa hizo, waliwafuatilia ndipo
majambazi hao waliposhuka kwenye pikipiki na kukimbia kwa miguu.
“Tumefanikiwa kuwakamata wawili wakiwa na pikipiki zao zenye namba
MC. 729 ATZ na MC.557 AZK. Wengine tunaendelea kuwasaka,” alisema.
Kuhusu bastola aina ya Browning, Sirro alisema ilipatikana eneo la
Kiwalani kwa Gude, baada ya polisi kupata taarifa za kuwepo kwa watu
wamekaa kichakani ambapo baada ya kuwafuatilia walikimbia na
kuidondosha.


0 comments :
Post a Comment