Nkupamah media:
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba.
.
Katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 40, kati yake ndipo zilipo nne za serikali zilizofanikiwa kupenya 100 bora.
Katika kundi hilo lenye shule 3,452 nchi nzima, shule za serikali
zilizofanikiwa kuwa kwenye 100 bora ni Ilboru ya Arusha iliyokuwa ya 53,
Kibaha ya Pwani iliyoshika nafasi ya 69, Mzumbe ya Morogoro ambayo ni
ya 71 na Kilakala ya Morogoro iliyoshika nafasi ya 94.
Shule ya kwanza kitaifa ni Kaizirege ya Kagera ikifuatiwa na Shule
ya Wasichana ya Alliance (Mwanza), St. Francis (Mbeya), Shule ya
Wavulana ya Alliance (Mwanza), Canossa (Dar es Salaam) na Shule ya
Wavulana ya Marian (Pwani).
Nyingine ni Alliance Rock Army (Mwanza), Shule ya Wasichana ya Feza
(Dar es Salaam), Shule ya Wavulana ya Feza (Dar es Salaam) na Uru
Seminary (Kilimanjaro).
Shule nyingine ni Msolwa (Morogoro), Precious Blood (Arusha), Abbey
(Mtwara), Shule ya Wasichana ya Marian (Pwani), Shule ya Wavulana ya
Tengeru (Arusha), Rosmini ya Tanga, Shule ya Wasichana ya Josiah
(Kagera), Katoke Seminari (Kagera), Don Bosco Seminary (Iringa) na St.
James Seminari ya Kilimanjaro.
Nyingine ni Loreto ya Mwanza, Kifungilo (Tanga), St. Joseph's
Iterambogo Seminari (Kigoma), St. Mary's Mazinde Juu (Tanga), St.
Amedeus (Kilimanjaro), Boniconsili Mabamba (Kigoma), Barbro-Johansson
(Dar es Salaam), Morning Star (Mwanza), Scolastica ya Kilimanjaro na
Kasita Seminari ya Morogoro.
Katika kundi hili pia kuna Shule ya Nyegezi Seminari (Mwanza),
Kanyigo ya Kagera, Joyland ya Kilimanjaro, Pandahill (Mbeya), St.
Mary's-Ulete (Iringa), Uwata (Mbeya), Holy Family (Mwanza), Queen of
family (Shinyanga), Itaga Seminari (Tabora), St. Marie Eugenie
(Kilimanjaro) na Shule ya Wasichana ya Peramiho ya Ruvuma.
Shule ya Olympus ya Mara, Shule ya Wasichana ya St. Clare
Biharamulo (Kagera), St. Ann's Seminari (Morogoro), St. Clara
(Kilimanjaro), St. Luise Mbinga (Ruvuma), Anderlek Ridges (Shinyanga),
Kandoto Sayansi (Kilimanjaro), Shule ya Wasichana Premier (Pwani) na
Mivumoni Islamic Seminari ya Dar es Salaam ni shule zilizo kwenye Kundi
la 50 bora.
Nyingine zilizo kwenye Kundi la100 bora ni Henry Gogarty ya Arusha,
Star (Arusha), Ilboru (Arusha), Carmel (Morogoro), Amani (Singida), St.
Peter Claver (Dodoma), Genda (Manyara), Shule ya Wasichana ya Mother
Teresa of Calcuta (Kilimanjaro), Huruma (Dodoma), Alpha (Dar es Salaam)
na Palloti (Singida).
Shule nyingine ni St. Joseph Millenium (Dar es Salaam), St. Francis
de Sales Mission (Tabora), Kowak (Mara), Maua Seminari (Kilimanjaro),
Famgi (Mwanza), Makoko Seminari (Mara), Lake (Mwanza), Kibaha (Pwani),
St. Joseph Seminary ya (Mwanza), Mzumbe (Morogoro), Charlotte
(Morogoro), St. Getrude Mlandizi (Pwani), Maria de Mattias (Dodoma) na
Geita Adventist ya Geita.
Nyingineni ni Sekondari ya Kitungwa ya Morogoro, St. Peter's
Seminari (Morogoro), St. Mary Goreti (Kilimanjaro), Bendel Memorial
(Kilimanjaro), Sanu Seminari (Manyara) na Shule ya Wasichana ya
Visitation (Kilimanjaro).
Sekondari nyingine ni Murutunguru (Mwanza), St. Rufino and Ronaldo
Agr (Kigoma), Stanley (Dar es Salaam), Loyola (Dar es Salaam), Tusiime
(Dar es Salaam), Oswe (Mbeya), Kidugala Lutheran Seminar (Njombe), Mbezi
Beach (Dar es Salaam), Ritaliza (Kilimanjaro) na Shule ya Wavulana ya
St. Stephen (Kilimanjaro).
Nyingine zilizo kwenye kundi hili ni ile ya Wasichana ya Kibosho ya
Kilimanjaro, Agape Lutheran Seminari (Kilimanjaro), Kilakala
(Morogoro), Shule ya Wasichana ya St. Francis of Assisi (Dodoma), Masama
(Kilimanjaro), St. Francis Xavier (Kigoma), Stella Matutina Lighano
Seminari (Ruvuma), Shule ya Wavulana ya Living Stone Seminari (Tanga) na
Trust Patrick (Arusha).
Katika mtihani huo ambao shule nyingi za mwisho ni zile za
serikali, watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na
asilimia 2.77, daraja la pili 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la
tatu 48,127 sawa na asilimia 13.56, daraja la nne 151,067 sawa na
asilimia 42.57 na wale wa sifuri ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
MAONI YA WADAU
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, akitoa
maoni yake kuhusiana na shule za sekondari za serikali kuendelea kufanya
vibaya katika mitihani ya kitaifa, alisema sababu kubwa ni mazingira
mabaya.
Mukoba alisema kinacholeta matokeo mabaya katika shule hizo ni
mazingira ya shule kuharibika huku kukiwa hakuna huduma muhimu kama
chakula, vitanda na maji.
"Kama mazingira ni mabovu vipaji vya wanafunzi hao vinazalishwaje?," alihoji Rais huyo wa CWT na kuongeza:
“Walimu nao wamekata tamaa, wanaona wabunge wanapewa magari wao
hakuna, kazi yao ni kutoa vipaji tu nao wameona huo ni wendawazimu.”
Alisema ili kunusuru elimu katika shule hizo, lazima serikali iboreshe mazingira kwa kuhakikisha huduma zote zinapatikana.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten Met), Cathreen Sekwao,
alisema sababu kubwa ya kushuka kwa elimu kwenye shule hizo ni huduma
maalum zilizopaswa kuwapo zimelegalega ikilinganishwa na hapo awali.
“Hakuna vitabu vya kutosha, hakuna walimu wazuri, mazingira yenyewe
siyo rafiki shule hazifanyiwi ukarabati, kwa ujumla hali siyo nzuri
katika shule hizi, zitawezaje leo kuitwa za vipaji maalum?,” alisema na
kuongeza:
“Tumekuwa tukiziangalia shule mpya za kata, hizi zimesahaulika hata matengenezo hazifanyiwi tena, zimechoka.”
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wamiliki na Mameneja wa Taasisi Binafsi za
Elimu Tanzania (Tamongsco), Benjamin Nkonya, alisema kufanya vibaya kwa
shule hizo ni suala la kisera ambalo limewafanya wanafunzi kubweteka
badala ya kusoma.
"Tumeshuhudia matokeo haya yameonyesha wazi kuwa mfumo wa zamani wa
divisheni umewaangusha wengi ule uliokuwa ukitumika ulikuwa unawabeba,"
alisema.
Pia alisema serikali inatakiwa kuona uwezekano wa kutumia mfumo wa
'vocha' ambao umefanikisha shule nyingi duniani ikiwamo Uganda ambayo
mzazi anachukua ada serikalini na kuchagua mwenyewe shule anayotaka.
Alisema utaratibu huo umepandisha hadhi za shule na kupunguza
gharama na kuwafanya wenye shule kushindana kuboresha shule zao ili
wazazi wazichague.
"Huu ni utaratibu mzuri badala ya serikali kumchagulia mtoto shule, mzazi anachagua mwenyewe," alisema.


0 comments :
Post a Comment