Nkupamah media:
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea.
Kubenea alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Umoja wa Wamiliki
na Wazalishaji wa Unga wa Sembe na Dona (Uwawase) jijini Dar es Salam.
Alisema tayari fedha hizo za mfuko wa jimbo zimeshafika na
kinachofanyika ni kupanga mikakati na kuchambua vipaumbele ambavyo fedha
hizo zitaelekezwa.
Alisema uongozi wa jimbo hilo umepanga kuhakikisha unashughulikia
kero na changamoto mbalimbali katika jimbo hilo, ikiwamo kuangalia namna
ya kutumia fedha za mfuko huo kuwawezesha wananchi wake kiuchumi.
Mbali na kupeleka katika kila kata, alisema wamepanga kusaidia
vikundi mbalimbali vya ujasiliamali katika miradi yao na hata
ikiwezekana walipe kwa riba ndogo ili wananchi wote katika jimbo hilo
wanufaike.
“Fedha za mfuko wa jimbo katika jimbo letu zimekwishafika.
Tumepanga kila kata wapate kwa ajili ya maendeleo. Pia tunataka vikundi
vitumie pesa hizo angalau hata kwa mkopo kwa riba ndogo ili izunguke na
watu wote wapate. Tunaamini kwa kufanya hivyo tutapunguza wategemezi
katika jimbo letu,” alisema Kubenea.
Kadhalika, alisema anatarajia kupeleka hoja binafsi bungeni ili
serikali ifikirie namna ya kuweka mpango wa kuwa inauza mahindi kwa
vikundi vya uwekezaji vya ndani badala ya kuuza nje ya nchi.
Mbali na hilo, pia aliiomba Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
kuhakikisha inawapatia maeneo ya kuweka mashine za kusagia wasagishaji
wa unga wa dona na sembe ili waondoke katikati ya mji.
Kwa upande wake, Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Jumanne
Amiri, alisema wamepanga kukutana na wafanyabishara hao jumatatu ya wiki
ijayo ili kujadiliana nao na kuona ni sehemu gani wanaweza kuwapatia
maneo ya kuweka mashine zao za kusaga.
0 comments :
Post a Comment