Askofu
wa Kanisa la God News for all Ministry, Dk. Charles Gadi, akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhu kabla ya
kuliombea taifa lipate mvua akiwa na wachungaji mbalimbali. Kulia ni
Mchungaji Palemo Masawe.
Mchungaji Martini Ndaki (kushoto), akizungumza katika
mkutano huo.
Meza kuu kabla ya maombi.
Askofu
Charles Gadi (wa tatu kutoka kushoto), akiongoza maombi ya kuliombea
taifa lipate mvua. Kutoka kushoto ni Mchungaji Denis Komba, Mchungaji
Martin Ndaki, Mchungaji Palemo Masawe, Mchungaji Denis Kumbilo,
Mchungaji James Manyama na Mchungaji Leonard Kajuna.
Na Dotto Mwaibale
ASKOFU
wa Kanisa la God News for all Ministry, Dk. Charles Gadi, ameliombea
taifa lipate mvua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa inayosababisha
kuongezeka kwa joto nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Askofu Gadi
alisema, mabadiliko hayo ya kijiografia yamesababisha kukosekana kwa
mvua za kutosha katika mwanzo wa masika wa mwezi wa tatu na kukithiri
kwa joto kutokana na dunia kuwa karibu na jua(Equinox).
Alisema
mvua za masika ni muhimu sana kwa kilimo, ufugaji, malisho ya wanyama
mwitu wa nchini, mazao ya kudumu kama vile kahawa, migomba, michai na
mito yote hayo yanategemea mvua za masika.
“Tukumbuke
kuwa kuna kipindi kirefu hupita tangu mvua za masika hadi kukutana na
za vuli ambapo ni karibu ya miezi mitano au sita pasipo na mvua, hivyo
kama kukiwa na uhaba wa mvua za masika maana kipindi cha ukame
kitaongezeka kwa miezi saba hadi miezi minane jambo ambalo ni hatari
sana kwa kilimo na wanayama wetu.
“Joto
la Equinox limekuwa kali kuliko wakati mwingine wowote ingawa
lilitarajiwa kuchemsha maji ya bahari ili mvua ziwe nyingi lakini hali
imekuwa kinyume, hivyo tunawaaasa watanzania wote bila kujali dini na
itikadi ya mtu kuungana kwa pamoja kumuomba mungu ili ukame huu
usiikumbe nchi yetu,” alisema Askofu Gadi.
Alisema
ni lazima kuomba ili ipatikane mvua za kutosha nan chi iweze
kujitegemea kwa chakula ili fedha ambazo zingetumika kuagiza chakula
nje ya nchi ziweze kutumika kwenye kuleta maendeleo ya kitaifa.
Aidha
Askofu Gadi aliishukuru Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA)kwa kuendelea
kutoa taarifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi na kijiografia
yanayosababisha kuongezeka kwa joto kwa kikwango kikubwa.
Askofu Gadi alifanya maombi hayo kwa kushirikiana na wachungaji wenzake ambao ni Mchungaji Denis Komba, Martin Ndaki, Palemo Masawe, Denis Kumbilo, James Manyama na Mchungaji Leonard Kajuna.
0 comments :
Post a Comment