Mshindi wa mbio za Kilometa 10 za
Kilimanjaro Marathon 2016, Vosta Peter (30) akishangilia mara baada ya
kumaliza. Mbio hizo za Kilometa 10 zilidhaminiwa na kampuni ya GAPCO na
kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mshindi wa kwanza kwa mbio za
walemavu kilomita 10, Vosta Peter (30) akipokea cheki ya Shilingi
Milioni Moja kutoka kwa kampuni ya GAPCO, wanaomkabidhi ni Meya wa
Manispaa ya Moshi Raymond Mboya (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Gapco Afrika Mashariki, Macharia Irungu (anayepiga makofi toka kushoto)
na Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO Tanzania, Vijay Nair. Picha na Cathbert
Kajuna wa Kajunason Blog.
——————————————————————————————–
Habari na Cathbert Kajuna.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
GAPCO Afrika Mashariki, Macharia Irungu amewataka wanamichezo
kujibidishe kwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri
katika mashindano wanayoshiriki.
Akizungumza mwishoni mwa wiki
mjini Kilimanjaro wakati wa Mashindano ya Kilimanjaro Marathoni 2016,
ambapo GAPCO ndiyo waliodhamini upande wa Walemavu, alisema kuwa
wanamichezo wengi walemavu na hata wasiowalemavu hujisahau sana kufanya
mazoezi ya kutosha jambo linalowafanya wengi wao kutoweza kufanikiwa
kushinda kwenye mashindano.
Aliongeza kuwa wao kampuni ya
GAPCO waliweza kujitolea kuwasaidia walemavu ili waweze kuonyesha vipaji
vyao japo mwanzo waliweza kuwasisitiza wafanye mazoezi na ndiyo maana
wameweza kufanya vyema.
“Napenda kuwaasa wanamichezo wale
walemavu na wasio walemavu, wapende kujitoa kufanya mazoezi ya kutosha
maana siri ya ushindi ni mazoezi wala hakuna muujiza unaoweza kukupa
ushindi kama haujajitoa kufanya mazoezi ya kutosha,” alisema Irungu.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Vijay Nair alisema wamefurahishwa
na mahudhurio ya watu wenye ulemavu waliojitoa kushiriki mashindano
hayo, na wao hawatawatupa wataendelea kuwa nao bega kwa bega.
Bw. Nair aliwaasa walemavu wawe
na moyo wa upendo na mshikamano ili waonyeshe mfano bora hata
wanapojitokeza kusaidiwa wafaidike kwa pamoja.
Mashindano ya mbio za Kilimanjaro
marathon za 10KM kwa walemavu zilidhaminiwa na GAPCO ambapo shindano
lilijumuisha baiskeli za walemavu zenye matairi matatu zenye viwango vya
kimataifa wapatao 60 kutoka Dar es Salaam, Arusha, Moshi na Zanzibar.
0 comments :
Post a Comment