Nkupamah media:
Meneja Masoko na Mawasiliano wa
LAPF, James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wao
uliofanyika Milenium Tower jijini Dar es salaam wakati alipoelezea
kuhusiana na mkutano wa mwaka wa wadau wa LAPF unaotarajiwa kufanyika
kwenye ukumbi wa AICC mwezi huu kwa sikU mbili jijini Arusha. Pichani
kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama Bw. Valerian Mablangeti.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia taarifa iliyotolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa
LAPF, James Mlowe wakati akizungumza nao katika ofisi za Shirika hilo
zilizopo Mkumbusho jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama
Bw. Valerian Mablangeti akiwafafanulia jambo waandishi wa habari wakati
wa mkutano huo kulia ni Bw. James Mlowe Meneja Masoko na Mawasiliano wa
LAPF.
………………………………………………………………………………..
MFUKO wa Pensheni wa LAPF
umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja na bilioni 87 za thamani ya
uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.
Hayo
yalibainishwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF James Mlowe
wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo asubuhi kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa
kufanyika Machi 10 na 11 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC
jijini Arusha.
Alisema LAPF imeendelea kupiga hatua kila mwaka ukilinganisha na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii hapa nchini.
”
LAPF imeweza kutoa mikopo ya masomo kwa watu 800 katika maeneo
mbalimbali nchini yenye thami ya sh.bilioni 1.2 jambo ambalo
tunajivunia” alisema Mlowe.
Akizungumzia
kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian
Mablangeti alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika kwa wadau wa
mfuko huo kupatiwa barua za mualiko.
Alisema
mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais-Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene na kuwa
mawaziri wengine wakaoshiriki kwenye mkutano huo ni Waziri wa Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na Naibu Waziri
Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Jafo Selemani .
Alisema
katika mkutano huo Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atatoa
taarifa ya hesabu za mfuko huo na pia kutakuwa na mada inayohusu afya
kutoka kwa Daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
0 comments :
Post a Comment