Mwenyekiti
wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva akimwagilia maua
mara baada ya kuwakabidhi mpira wa Mita 100 kwa wanakikundi cha Green
Garden jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo akizungumza kwa mwandishi
wetu mara baada ya kupewa msaada wa mpira wenye mita 100 utakao
wawezesha kumwagilia maua kwa urahisi zaidi tofauti na mwanzo na
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), (kushoto) Zefrin Lubuva akikabidhi Mpira wa Mita 100 kwa wanakikundi cha Green Garden kilichopo Mbuyuni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM) (Mwenye kitambulisho), Zefrin Lubuva akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi mpira wa mita 100 jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM) (mwenye kitambulisho), Zefrin Lubuva akipewa
maelekezo na Mwenyekiti wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo mara
baada ya kukabidhi mpira wa kumwagilia maua katika kikundi hicho
kilichopo Mbuyuni jijini Dar es Salaam.
Wanakikundi wakiufungua mpira kwaajili ya kuanza kazi mara baada ya kukabidhiwa mpira wa mita 100 leo jijini Dar es Salaam.
WANAKIKUNDI
cha Green Garden ambao wanafanya biashara uuzaji na utunzaji maua
pembeni kidogo ya kituo cha mabasi cha Mbuyuni jijini Dar es Salaam
wapewa mpira kumwagilia maua wa Mita 100 na Mwenyekiti wa Serikali za
Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva.
Mwenyekiti
wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva amesema kuwa
ameona vyema kutimiza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi wa
viongozi wa serikali za mtaa kwa wanakikundi hicho kwani aliwaahidi
kuwasaidi amesema Mwenyekiti huyo wakati wa kukabidhi mpira wa
kumwagilia wa mita 100 leo pembeni ya kituo cha mabasi ya Mbuyuni jijini
Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo ameashukuru Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva kwa kutimiza ahadi ahadi yake.
"Tulikua
na mpira ambao ulikuwa umetoboka tulijitahidi kuziba na makaratasi ili
usivuje sasa tumepata mpya tena wa mita 100 sasa tutakuwa kukijitahidi
kutunzaji wa maua vizuri"
Mombo
amesema kuwa kikundi hicho kimeanzishwa mwanzoni mwa mwaka 1985 mpaka
sasa wapo tuu kwa sababu ya kujitafutia liziki ikiwa wanapata changamoto
mbali mbali hasa za kukosa wateja kwa mda mwingine.
0 comments :
Post a Comment