Nkupamah media:
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya
Taifa ya mpira wa miguu wanawake “Twiga Stars” wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura (hayupo pichani) alipowatembelea kambini kwao leo jijini Dar es
Salaam.Twiga Stars inatarajiwa kucheza mechi na Timu ya Taifa wanawake
ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa tarehe 4 katika uwanjja wa Taifa.
Picha na WHUSM
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na
wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars”
alipowatembelea kambini kwa leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Nkenyenge na Mjumbe wa Baraza
la Michezo la Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia).
Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Selestine Mwesiga akitoa shukura kwa
Serikali kutokana na jitihada zake za kuitafutia wadhamini Timu ya Taifa
ya Mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars) wakati Naibu Waziri wa Habari,
Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura(wapili kutoka
kushoto) alipo watembelea wachezaji wa Timu hiyo leo jijini Dar es
Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bi.
Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia). Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo
Makoye Nkenyenge.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akisalimiana
na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars”
(Nasra Juma) alipowatembelea kambini kwao leo jijini Dar es Salaam.
Katikati ni mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Jeniffer
Mmasi Shang’a.
Mjumbe wa Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a. akisalimiana na Kocha wa Timu ya
Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” Bibi. Nasra Juma
wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) kambini kwao leo jijini
Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shijja,WHUSM
Serikali kupitia Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa motisha kwa wachezaji wa Timu
ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake(Twiga Stars) ikishinda katika
mchezo wake dhidi ya Zimbabwe unatarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa tarehe
4 machi katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Haya yamebainishwa na Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia James Wambula
alipotembelea kambi ya Timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wachezaji wa Twiga
Stars, Wambura amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa
michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo zitatumika kama motisha
kwa wachezaji hao.
Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa
iwapo timu hiyo itaibuka na ushindi katika mechi yake dhidi ya Zimbabwe
kila mchezaji atapata gawio la sh. Laki tatu kama mptisha na kuongeza
kuwa itafanyika hivyo hivyo katika mchezo wa marudiano utakaochezwa
nchini Zimbabwe.
Aidha alitumia fursa hiyo
kuwaomba wadau wa michezo kuzidi kujitokeza na kuisaidi timu hiyo ikiwa
ni pamoja na kuhudhuria kwa wingi katika mechi ya tarehe 4 machi dhidi
ya Zimbabwe itakayochezwa katika uwanja wa Taifa.
Aliongeza kuwa msaada zaidi
unahitajika ili kuiwezesha timu hiyo kukidhi mahitaji yake muhimu,hivyo
alitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoa michango yao kupitia Twiga
Specila Fund, Akaunti na: 20110001677 iliyoko NMB tawi la Bank House
jijjini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
TFF Selestine Mwesiga ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za
kuhakikisha Twiga Stars inapata huduma muhimu ikiwemo motisha kwa
wachezaji na benchi la ufundi.
Mwesiga pia amewapongeza wadau
wote waliojitolea kusaidi timu hiyo ambapo amesema kujitokeza kwa wadau
hao kunaongeza morali ya wachezaji.
Msaada huo wa shilingi milioni 15
umetolewa na wadau watatu ambapo mmoja aliyechangia sh. Milioni 3
aliomba jina lake lihifadhiwe, wengine ni Kampuni ya ASAS sh. Milioni 2
na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) sh. Milioni 10.
0 comments :
Post a Comment