Mwanafunzi
wa shule ya SEKONDARI NAMABENGO ambaye hakufahamika jina akionyesha
kidonda anachouguza kutokana na fimbo ambazo wanapigwa na mwalim mkuu
msaidizi wa shule hiyo SHAIB CHAMPUNGA.
Wanafunzi wa shule ya sekondari namabengo wakiwa wamekaa na kumsikiliza afisa elimu wa wilaya hiyo ambaye hayupo pichani .
………………………………………
Na Gidion Mwakanosya.
Wanafuzi
106 wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Namabengo wilaya ya
Namtumbo mkoani Ruvuma wameandamana kwenda kumwona mkuu wa mkoa Said
Mwambungu kumpelekea malalamiko dhidi ya vitendo vya
udharirishaji wanavyofanyiwa na makamu mkuu wa shule hiyo Shaibu
Champunga.
Mwalimu
huyo anadaiwa kutoa vitisho na lugha za matusi kwa wanafunzi,kuchapwa
viboko visivyo na idadi,kuingi kwenye bweni la wanafunzi wa
kike nyakati za usiku bila kuongozana na matroni na kuwalazimisha kutaka kufanya mapenzi pamoja na kuwazuia wanafunzi wa kike kulala bwenini.
kike nyakati za usiku bila kuongozana na matroni na kuwalazimisha kutaka kufanya mapenzi pamoja na kuwazuia wanafunzi wa kike kulala bwenini.
Kutokana
na malalamiko ya wanafunzi hao walitaka kwenda kumwona mkuu wa mkoa ili
aweze kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero zao juhudi
za kutaka kuonana na mkuu huyo wa mkoa ziligonga mwamba wakati wamesha tembea kwa miguu kilomita Zaidi ya 16 kabla ya kufikla Songea mjini ambako askari polisi wakiongozwa na mkuu wa polisi wilaya ya Namtumbo kuwazuia wasiendelee na maandamano.

Wanafunzi
hao walikutwa kijiji cha Mlete kilicho nje kidogo ya manispaa ya
Songea ambapo askari polisi waliwaamuru wasimame ndipo mkuu wa polisi
wilayani humo aliwataka waeleze sababbu za kufanya maandamano bila
kibali,wanafunzi hao walimweleza kuwa kila mtu anahaki ya kuongea kwa
kuwa walishatoa malalamiko yao kwa mkuu wa shule lakini hayakusikilizwa
hivyo waliona vema wakakutane na mkuu wa mkoa labda ataasikiliza.
Muda
mfupi baadae alifika katibu tawala wa Namtumbo Alkwine Ndimbo na
kusikiliza malalamiko mengi ya wanafunzi ambapo walimweleza kuwa
makamu mkuu wa shule ya Sekondari Shaibu Champunga hawamtaki shuleni hapo kwa sababbu anatuhumiwa kuwa na lugha chafu zenye kejeri ikiwa ni pamoja na kuwataja kwa majina wanafunzi wanaodaiwa kuwa na ugonjwa wa Ukimwi.

Walisisitiza
kuwa shule hiyo haina miundombinu mizuri ambapo wamedai kuwa vyoo ni
vibovu havifai kutumika,baadhi ya madarasa hayana sakafu
paja na kwamba wanalazimika kwenda umbali mrefu kufuata maji.
paja na kwamba wanalazimika kwenda umbali mrefu kufuata maji.
Baada
ya viongozi hao kusikiliza malalamiko ya wanafunzi waliwataka warudi
shuleni ili wakatoe maamuzi mbele ya wanafunzi wote pamoja na
walimu jambo ambalo wanafunzi walikubali na kusitisha maandamano.
walimu jambo ambalo wanafunzi walikubali na kusitisha maandamano.
Kwa upande wake ofisa elimu wa sekondari wilaya ya Namtumbo Patrick Atanasi ambaye aliyefika kwa kuchelewa wakati tayari katibu tawala wa
wilaya hiyo Ndimbo ameshakubaliana na wanafunzi warudi shuleni alisema
kuwa kitendo walichofanya wanafunzi cha kuandamana ni kosa kubwa na
utovu wa nidhamu na inapaswa kilaaniwe na kuwachimba mkwara wasirudie
tena jambo lililowafanya wanafunzi kuguna.
Jitihaa
za kumpata kamanda wa polisi ofisini kwake na kwa njia ya simu hakuzaa
matunda ili kudhibitisha tukio hilo badala yake alitafutwa
mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai moa wa Ruvuma Levokatus malimi alikili kutokea kwa tukio hilo mbalo alidai kuwa limeshaanza kufanyiwa kazi.
mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai moa wa Ruvuma Levokatus malimi alikili kutokea kwa tukio hilo mbalo alidai kuwa limeshaanza kufanyiwa kazi.
0 comments :
Post a Comment