Uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia
mahafali ya wanafunzi waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT ) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana mchana chuoni hapo
jijini Dar es Salaam, ambapo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa
alikuwa amealikwa na wanafunzi kama mgeni rasmi.
Mahafali hayo yalizuiwa jana saa 6 mchana ikiwa ni saa mbili kabla ya muda kuanza
Tangazo
lililobandikwa chuoni hapo na kushuhudiwa na wanahabari likiwa
linamnukuu Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Apollinary
Kamuhabwa liliwataka wanafunzi hao kutoweka mikusanyiko ya aina yoyote
chuoni hapo.
Profesa
Kamuhabwa kupitia tangazo hilo aliwaonya wanafunzi hao kutojihusisha na
masuala ya siasa wawapo chuoni kama ilivyo kwa watumishi wa umma.
Jitihada
za waandishi wa habari kuzungumza na uongozi wa chuo hicho ili kupata
ufafanuzi ziligonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa hawakualika mkutano na
waandishi wa habari.



Blogger Comment
Facebook Comment