Wanamgambo nchini Ufilipino waliotangaza kulitii kundi la Islamic State wamewatorosha kutoka jela wapiganaji wenzao nane wakati wa uvamizi uliofanywa kwenye gereza moja katika mji ulio kusini mwa Marawi nchini humo.
Polisi wanasema kuwa takribani wapiganaji 20 kutoka kundi la Maute walivamia gereza la Lanao del Sur Jumamosi usiku na kuwapokonya silaha walinzi waliokuwa wanalinda gereza hilo.
Wanamgambo hao waliotoroshwa walikamatwa wiki iliyopita baada ya utawala wa serikali ya Ufilipino kuwakamata wakati wakisafirisha vilipuzi vya kutengenezewa kwa kutumia gari lao.
Aidha, takriban wafungwa wengine15 walitumia fursa hiyo kutoroka jela.
Na Regina Mkonde
0 comments :
Post a Comment