Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump amesema kuwa atabuni mfumo ambao utasaidia serikali ya nchi hiyo kudhibiti uhamiaji.
Akizungumza wakati wa kampeni katika jimbo la Lowa nchini humo, Trump alisema kuwa mfumo huo utasaidia kuwatimua watu ambao wanaishi nchini Marekani licha ya muda wa visa zao kumalizika.
Pia alirejelea wito wake wa kujengwa ukuta kati ya mpaka wake na Mexico ili kuwazuia wahamiaji.
Na Regina Mkonde
0 comments :
Post a Comment