Klabu
ya Tottenham Hotspur inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) imepata
majanga baada ya kujulikana kuwa inaweza kumkosa mashambuliaji wa klabu
hiyo, Harry Kane kwa miezi mwili.
Sababu
ya Kane kuwepo nje ya uwanja kwa muda huo ni majeraha ambayo aliyapata
katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Sunderland ambapo alitolewa katika
dakika ya 87 na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Baada
ya zipimo, taarifa zinaonyesha kuwa alipata majeraha katika kifundo cha
mguu na anaweza kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili lakini Tottenham
bado haijatoa taarifa rasmi kwani inasubiri afanyiwe vipimo kwa mara ya
pili na baada ya hapo itatoa taarifa rasmi.
Kama
Kane atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mwili basi ataikosa michezo mitatu
ya EPL dhidi ya Manchester City, Leicester City na Arsenal.


0 comments :
Post a Comment