WANAFUNZI 24,616 WAKOSA NAFASI KUJIUNGA VYUO VIKUU



Dar es Salaam. Wanafunzi  24,616 kati ya 55,347 waliomaliza kidato cha sita wamekosa nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu kutokana na ushindani kwenye baadhi ya kozi, jambo lililoilazimu  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuongeza muda wa udahili.

Uamuzi huo wa TCU, unakuja siku moja baada ya kulegeza vigezo vya wanafunzi wa stashahada kujiunga na shahada ya kwanza katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.

Kaimu Katibu Mkuu wa TCU, Eleuther Mwageni alisema wanafunzi waliokosa nafasi walikuwa na sifa stahiki, hivyo tume inaongeza muda wa siku 11 kuanzia Septemba 12 hadi 23 ili kutoa nafasi kwa waliokosa vyuo kufanya maombi upya kwenye kozi tofauti na za awali.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment