NCHI HAINA DAWA MAHOSPITALINI, SERIKALI NA PAP WANAHAHA KUFUJA MABILIONI YA WATANZANIA
Gazeti
 la The Citizen limeandika Juu ya Suala la Ukosefu wa Madawa Katika 
Hospitali zote Nchini. Hii ni Habari Mbaya na Kuogopesha Kwa Watanzania 
Wote.
Sababu
 Kubwa ya Kukosekana Kwa Madawa kwenye Mahospitali nchi Nzima ni 
Serikali kukosa Fedha. Serikali imeipa Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) 
32% Tu ya Fedha ambazo ilipaswa kutoa Kwa MSD. Serikali ilipaswa kutoa 
Shilingi Bilioni 62.5 Kwa MSD Katika Kipindi cha Mwezi Julai mpaka 
Septemba 30. Lakini mpaka Leo imeipa MSD Kiasi Cha Bilioni 20 tu.
Uchunguzi
 Umeonyesha mpaka Septemba 16 MSD walikuwa na Tembe za Vidonge vya 
Paracetamol 170,000 Tu Katika Bohari Yao ya Mbeya. Huku Nchi Hospitali 
zikiwa hazina Kabisa Tembe Hizo. Hali ikiwa Ni Hivyo Hivyo Hivyo Katika 
Dawa za Ukimwi (ARVs), Vifaa Tiba kwaajili ya Mama Na Mtoto, Dawa za 
kipindupindu nk.
Katika
 Wakati ambao imegundulika tumelipa Kampuni ya Kitapeli ya PAP kwenye 
Sakata la Escrow zaidi ya Dola Milioni 245 Sawa Na Shilingi Bilioni 530 -
 Kiasi hiki Cha Fedha Ni zaidi ya Mara Mbili ya Bajeti ya Shilingi 
Bilioni 251 ya MSD Kwa Mwaka. Na tukilipa Bilioni 320 tunazodaiwa Baada 
ya Hukumu ya ICSID tutakuwa tumelipa zaidi ya Mara Tatu ya Bajeti ya MSD
 Kwa Mwaka.
Serikali ya CCM ionyeshe kuwa inawajali Wananchi wake Kuliko inavyowapenda Mafisadi wa PAP.
Zitto Kabwe Ruyagwa
Septemba 26, 2016



0 comments :
Post a Comment