PROF LIPUMBA- MIMI NI MWENYEKITI HALALI WA CUF,NIKO NGANGARI KINOMA..!!!



 
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi, (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amerudia kueleza sababu za uamuzi wake kujiuzulu uenyekiti wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Amesema ukiukwaji wa Katiba ya CUF kwenye baadhi ya mambo ilimchefua na kulazimika kufanya uamuzi huo mgumu katika kipindi kigumu, lakini akasema hadi sasa yeye ndiye Mwenyekiti halali wa CUF, akitaka wanaCUF kudharau mambo aliyoyaita ya uzushi kuhusu chama hicho na yeye kwenye mtandao.

Alisema hayo jana mjini hapa alipozungumza na wanachama wa katika kikao cha ndani akiwa katika ziara ya siku mbili kabla ya kwenda Lindi kuendelea na ziara hiyo.

“Ndugu zangu wanachama, nimetengua rasmi uamuzi huo wa kujiuzulu baada ya kupandwa na jazba kutokana na uvunjwaji wa Katiba yetu, sasa tuendelee kujenga chama chetu kwani nimerudi. Mimi niko ngangari kinoma, msiamini mambo ya kwenye mitandao niko ngangari,” alisema Lipumba.

“Msimamo na Mwongozo wangu Profesa Ibahim Lipumba ni Mwenyekiti halali wa CUF na mwanachama halali na huu ni msimamo na mwongozo ambao umesimamia Katiba yetu kwani haki ya kujiuzulu ninayo na ya kutengua ninayo, hapakuwa na sababu ya kufika hapa,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment