Mganga Mkuu wa Wilaya ya Singida Vijijini, Dk. Erick Bakuza ameandika barua ya kuacha kazi
Dk.
Bakuza amechukua uamuzi huo ikiwa ni siku chache tangu alipopewa adhabu
ya kuwekwa mahabusu na Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Rehema Nchimbi.
Dk.
Nchimbi alitoa amri ya kukamatwa kwa daktari huyo kutokana na kuzuka
ugonjwa wa kipindupindu ambao ulisababisha vifo vya watu wawili mwishoni
mwa mwaka jana.
“Ni
kweli amewasilisha barua ya kuacha kazi lakini ninavyojua mimi si kweli
kwamba ameacha kazi kutokana na adhabu aliyopewa na Mkuu wa Mkoa ya
kuwekwa ndani.
“Kwanza
ujue hakuwekwa ndani, na ameamua kuacha kazi kwa sababu amepata sehemu
nyingine ambayo anaona ina maslahi anayohitaji yeye,” alisema.
Juhudi za kumpata Dk. Bakuza kuzungumzia hatua yake hiyo hazikuzaa matunda.
Kauli ya Mkuu wa Mkoa
Wakati
Mkurugenzi huyo akisema kwamba Dk. Bakuza hakuwekwa ndani, Mkuu wa Mkoa
huyo, Dk. Nchimbi alithibitisha kwamba aliwekwa ndani kwa saa tatu.
“Mimi
nilitoa amri ya kukamatwa Daktari huyu na aliwekwa chini ya ulinzi kwa
saa tatu.Nilimuweka ndani kwa sababu ya mazingira ambayo niliyakuta
nilipokuja kuanza kuitumikia nafasi niliyoteuliwa ya ukuu wa mkoa, na
nitatetea uamuzi wangu huo.
“Niliamuru
akamatwe kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu, kesi ya
kwanza ya kuwapo kwa mgonjwa wa kipindupindu iliripotiwa Novemba 26,
mwaka jana.
“Utaratibu
unajulikana wazi kwamba ikifika kesi tano DMO (Mganga Mkuu wa Wilaya)
anatakiwa atoe taarifa kwa MRO (Mganga Mkuu wa Mkoa).
“Desemba 4 hakutoa taarifa, ilipofika Desemba 16 vikatokea vifo viwili hakutoa taarifa hadi Desemba 18 ndipo akatangaza.
“Nikaona
hakuwa makini katika kazi yake kwa sababu alipaswa kutangaza mapema ili
tuchukue hatua za kudhibiti ugonjwa huo na naamini hata hivyo vifo
visingetokea,” alisema.
Dk. Nchimbi alisema suala la kipindupindu halipaswi kuchukuliwa kisiasa na kwamba lenyewe lipo kitaalamu zaidi.
“Kuna
taratibu ambazo hufuatwa lazima tupate evidence ya kutosha, watu
wachukuliwe vipimo, yeye alinyamaza kimya. Wataalamu walipokwenda
kuchunguza wakagundua kuna kipindupindu kwenye wilaya yake,” alisema.
Aliongeza: “Kwa hali hiyo niliona hakuwa makini katika kazi yake, hivyo nilitaka kumshtua tu awe makini, hakuwa makini.
“Katika
hali ya kawaida angesema mapema tungechukua hatua mapema, tungetibu
maji, tungesafisha visima na hata vifo visingetokea,” alisema.
0 comments :
Post a Comment