Umoja
 wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umesema kutokana na kushamili
 kwa ubabe, udikteta na ung’ang’anizi  wa madaraka ipo siku viongozi wa 
upinzani wataondolewa kwa nguvu na aibu.
Hayo
 yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, jijini Dar 
es salaam baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji 
kilichokutana kutathmini ushindi wa uchaguzi.
Shaka
 amesema kuwa watanzania wataendelea kuiamini CCM kwa mambo mengi, 
ikiwemo kuleta uhuru na mapinduzi, sera, uongozi na utawala, kujali na 
kutazama maslahi mapana kwa manufaa ya umma na pia tabia ya utii wa 
sheria na kuheshimu katiba bila shuruti.
“Viongozi
 ving’ang’anizi wa madaraka ya kisiasa ni hatari kukabidhiwa dhamana ya 
madaraka na dola, ikitokea bahati mbaya siku moja wakapewa dhamana hiyo,
 hawatapisha wengine na huo utakuwa ni mwanzo wa kutikisika misingi ya 
utaifa, mshikamano na amani ya nchi,”amesema Shaka.
Aidha,
 Shaka amesema kuwa inashangaza kuwaona viongozi wa kisiasa ,akiwemo 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif 
wakijenga himaya ndani ya vyama vyao huku wakidaiwa kufanya ubabe katika
 uongozi wao.



0 comments :
Post a Comment